ADA Tadea wafanya uzinduzi Bara, Visiwani wadhamiria kuufuta umaskini, maradhi kupitia rasilimali zilizopo nchini

Chama cha Siasa cha ADA Tadea kimefanya uzinduzi wa kampeni kwa upande wa Tanzania Bara na Visiwani huku wagombea wake wakisema iwapo Watanzania watawapa ridhaa kuanzia ngazi ya udiwani hadi Urais Oktoba 28, mwaka huu wanatarajia kutekeleza miradi mingi na kuufuta kabisa umaskini nchini, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungazo wa Tanzania kupitia chama hicho, John Shibuda amesema wamedhamiria kitenda mambo mengi kwa maendeleo ya wote.

Pia amesema, ADA Tadea hawana uadui na chama chochote cha kisiasa nchini badala yake maadui wakubwa wa chama ni umaskini na maradhi.

Mgombea huyo amesisitiza kuwa,dhamira yao nyingine ni kuhakikisha utawala bora unapatikana nchini.

Aliyasema hayo Septemba 27,mwaka huu wakati akizindua kampeni za chama hicho kitaifa wilayani Maswa mkoani Simiyu.

Amesema,wao ADA Tadea hawana tatizo lolote na vyama vingine vya siasa bali tatizo lao ni mapambano dhidi ya mambo tajwa juu.

Shibuda amesema, wamejipanga kuondoa maadui hao kwa ustawi na maendeleo ya jamii ya watanzania ambapo amewaomba watanzania kumpigia kura ili awezea kuwaletea maendeleo kwa haraka.

Amesema, mambo mengine ni juu ya utawala wa sheria wakati wote kwa wananchi na watendaji wa umma ikiwemo siasa safi na atawajibika kwa uwazi bila upendeleo kwa mtu au kundi lolote.

Lydia Mbuke Bendera ambaye ni mgombea ubunge jimbo hilo kupitia ADA Tadea amewaasa wananchi kutokubali kupoteza kura zao badala yale Oktoba 28, mwaka huu
wamchague ili akazipatie ufumbuzi kero zinazowakabili katika nyanja zote.

Wakati huo huo, mgombea Urais Zanzibar kupitia chama hicho amehaidi iwapo wananchi watampa ridhaa na wagombea wengine wa chama hicho watahakikisha sekta ya kilimo,afya na fursa za ajira kwa vijana zinawaneemesha wote.

Juma Ali Khatibu ambaye ni mgombea Urais Zanzibar ameyasema hayo wakati alipokuwa akizindua kampeni za chama hicho katika Kiwanja cha Magae Songea jijini Zanzibar.

Pia amewataka wenzake kutoingiza siasa katika dini kwani masheikh wanaweza kufanya kazi yao ya kuwaelimisha waumini wao na wanasiasa kutumia majukwaa yao kunadi sera zao ili mwananchi achague kiongozi atakayeleta maendeleo ya nchi.

Mgombea huyo amesema kuwa, endapo watachaguliwa kuingia madarakani watahakikisha wanaendeleza miradi yote mikubwa iliyoanzishwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Awamu ya Saba chini ya Rais  MohDkt.Aliammed Shein ingawa wapo watu wanaobeza miradi hiyo.

Kwa upande wake Mgombea Mwenza ,Hassan Kijogoo amewataka wananchi kuendeleza amani ya nchi yao na kuomba wananchi wawape kura ili wakawatumikie kwa uadilifu.

No comments

Powered by Blogger.