Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Barbara Gonzalez afanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF),

Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Barbara Gonzalez amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad kwenye makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo jijini Cairo, Misri.

Baada ya kukutana Rais Ahmad amempongeza Barbara kwa kupata nafasi hiyo kubwa, lakini pia kumtaka kuitumia vyema ili kuonesha kwamba anaimudu kazi hiyo ambapo itakuwa ni moja ya njia ya kuhamasisha wanawake wengine kushika nafasi za juu za uongozi wa soka.







Kwa upande wake Barbara amemshukuru Rais Ahmad na CAF kwa mapokezi mazuri, lakini pia kuahidi kufanya kazi kwa bidii ili kusaidia kukuza soka la Afrika.

Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa CAF, Abdelmounaïm Bah, Makamu Katibu Mkuu wa CAF, Anthony Baffoe na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Mulamu Nghambi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news