Ajali ya basi lililopinduka yasababisha majeruhi 22, wengine wavunjika miguu

BASI la abiria lenye namba ya usajili T.629 CQC Scania lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Mwanza limeacha njia na kupinduka kisha kusababisha majeruhi na uharibifu wa gari hilo na baadhi ya mali za abiria, leo Septemba 10, 2020.

Ajali hiyo imetokea katika maeneo ya Inyala – Mablock, Kata ya Inyala mkoani Mbeya,  Barabara kuu ya Mbeya – Njombe huku chanzo kikiwa ni mwendokasi wa dereva.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema abiria 22 wamepata majeraha sehemu mbalimbali kati yao 12 ni wanaume na 10 ni wanawake na kwamba baadhi yao wamevunjika miguu.

 Basi mali ya Kampuni ya Isamilo Express likitokea Mbeya kwenza Mwanza na likiendeshwa na dereva aitwaye Kini Daud Malimi (51) mkazi wa Igoma Mwanza iliacha njia , kupinduka na kusababisha majeruhi na uharibifu wa gari hilo na baadhi ya mali za abiria, Taarifa mpya soma hapa.

Katika ajali hiyo abiria 22 wamepata majeraha sehemu mbalimbali kati yao 12 ni wanaume na 10 ni wanawake ambapo majeruhi nane kati yao wanaume watano na wanawake watatu wamepelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na wengine 14 kati yao saba ni wanaume, na saba ni wanawake wanaendelea kupata matibabu Kituo cha Afya Inyala.

Chanzo cha ajali ni uzembe wa  dereva kutaka kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake bila kuchukua tadhari pamoja na mwendo kasi katika eneo lenye mteremko mkali," ameyabainisha hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Matei.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news