AMSHA AMSHA YA UHURU FM VISIWANI ZANZIBAR YAJA NA MAJIBU YA KESHO

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Visiwani Zanzibar kimesema maandalizi ya Uzinduzi wa kampeni za CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu kesho zimekamilika kwa zaidi ya asilimia 100.

Katibu wa Kamati Maalum ya Nec Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Catherine Peter amesema hayo katika mahojiano maalum na Uhuru Fm leo.

Catherine amesema, uzinduzi huo wa kampeni utakuwa wa tofauti kulinganisha na kampeni zilizopita kutokana na asilimia kubwa ya wananchi kumkubali mgombea urais ambaye CCM imempa ridhaa ya kugombea nafasi ya urais visiwani Zanzibar.

Aidha, Catherine amesema wananchi wa Zanzibar wakipiga kura leo mgombea urais Dkt.Hussein Mwinyi ataondoka na ushindi wa kishindo kwa kuwa licha ya kukubalika kutokana na historia yake katika kazi, pia ana roho nzuri.

Pia amesema, namna ilani ya uchaguzi iliyotekelezwa kwa miaka mitano iliyopita chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein ,wana kila sababu ya kukichagua Chama Cha Mapinduzi.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Kuu Maalum ya CCM, Dkt. Khalid Mohamed amesema, Zanzibar imepaa kiuchumi na iwapo Wazanzibar watampa ridhaa Dkt. Mwinyi atafanya majabu kama kauli mbiu inavyosema "Yajayo Yanafurahisha".

Amesema, kwa sasa Zanzibar utekelezaji wa ilani inatosha umefanyika kwa kiwango cha juu ambapo shule, barabarani, hospitali na huduma zingine zimeimarika maeneo mengi hivyo Wazanzibar wana kila sababu ya kuchagua CCM.

Kidawa Saleh ni miongoni mwa Mjumbe wa Kamati Kuu Maalum ya CCM Zanzibar-Nec amesema, wanawake wana mambo mengi ya kueleza namna CCM katika ilani yake ilivowapa nguvu ikiwa ni pamoja na kupata nafasi mbalimbali za maamuzi ndani ya Serikali

Kidawa amesema, anaimani kubwa na Serikali ya CCM Zanzibar kwa kuwa wanawake walikuwa wakihangaika katika mambo mengi ikwemo afya na masuala ya shule, lakini kwa sasa hali imekua shwari katika maeneo yote.

Uhuru Fm pia imezungumza na baadhi ya viongozi wa CCM Pemba na Unguja ambapo wamesema hali ya kisiasa katika maeneo yao na wananchi wanasubiri siku ya uchaguzi ili kumpa ridhaa Dkt. Mwinyi ili aongoze kwa miaka mitano.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news