Moto waua wanafunzi 10, Serikali yaifunga Shule ya Msingi Byamungu Islamic

SERIKALI ya Mkoa wa Kagera imetangaza kuifunga kwa wiki moja Shule ya Msingi Byamungu Islamic ya wilayani Kyerwa mkoani humo.

Brigedia Jenerali Marco Gaguti ambaye ni mkuu wa mkoa huo amesema amefikia uamuzi huo ili kupisha Tume ya Uchunguzi yenye watu sita kufanya uchunguzi wa nini chanzo cha ajali hiyo iliyotokea leo na kusababisha vifo vya watoto 10 huku wengine wakijeruhiwa.

Amesema,shule hiyo haina wanafunzi wa darasa la saba ambao wana mtihani wa Taifa, hivyo "naifunga kwa wiki moja kuanzia sasa (leo) ili uchunguzi wa kina kuhusu ajali hii uweze kufanyika, lakini pia wanafunzi waweze kuungana na familia zao kwa ajili ya kupewa faraja ili waweze kusahau tukio lililotokea,"amefafanua Mkuu huyo.

RC huyo amesema pia amesitisha huduma ya malazi katika shule hiyo hadi maelekezo yatakapotolewa baada ya uchunguzi kufanyika huku akivitaka vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo kufanya mapitio upya ya shule za bweni zote za mkoani humo ili kuhakiki kama zina vibali halali vya Serikali vya kuruhusu malazi katika mabweni.

Ajali hiyo ya moto ambayo imetokea leo imesababisha vifo vya watoto 10 huku wengine wakijeruhiwa, huku ikielezwa kuwa, imekuwa vigumu kutambua miili ya watoto hao baada ya kuteketea vibaya hadi vichukuliwe vipimo vya vinasaba. Hayo yakiwa ni kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news