NEC yatoa maamuzi rufaa zingine za ubunge, udiwani

"Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika kikao chake cha jana tarehe 12 Septemba, 2020 imepitia, imechambua na kuzifanyia maamuzi rufaa za wagombea Ubunge na Udiwani zilizowasilishwa na wagombea kupitia kwa wasimamizi mbalimbali wa uchaguzi nchi nzima.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles akisoma taarifa kwa umma kuhusu rufaa za wagombea Ubunge na Udiwani Jijini Dar es Salaam leo tarehe 13 Septemba 2020.

"Rufaa hizo zimewasilishwa chini ya Kifungu cha 40 (6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kilichosomwa pamoja na kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ambacho kinatoa fursa kwa wagombea wa Ubunge na Udiwani kukata rufaa wanapokuwa hawajaridhika na uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi kutokana na pingamizi zilizowasilishwa;

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt.Wilson Mahera Charles ameyasema hayo leo Septemba 13, 2020 jijini Dar es Salaam ikiwa ni utaratibu wa tume kutoa matokeo ya rufaa mbalimbali baada ya kuzipitia na kuzichambua kwa kina.

Aidha, chini ya kanuni ya 32 (3) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020, ikisomwa pamoja na kanuni ya 30 (3) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2020, tume inaweza kukubali au kukataa rufaa hizo.

"Katika kikao hicho, tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi jumla ya rufaa 50, kati ya hizo rufaa nne ni za wagombea ubunge na 46 ni za wagombea udiwani. Kwa upande wa rufaa za wagombea ubunge, tume imekataa rufaa zote bbe ambazo ni za wagombea ambao uteuzi wao ulitenguliwa.Kwa hiyo, wagombea hao wanaendelea kutokuwa kwenye orodha ya wagombea. Rufaa hizo ni kutoka kwenye Jimbo la Babati Mjini.

Aidha, tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 46 za madiwani, kama ifuatavyo;

"Tume imekubali rufaa 25 na kuwarejesha wagombea udiwani katika orodha ya wagombea. Rufaa hizo ni kutoka kwenye kata za Changaa (Kondoa), Kichonda (Liwale),Kisima (Same Magharibi),Kibada (Kigamboni), Utende (Katavi),Myamba (Same Mashariki), Buswelu (Ilemela),Kiseke (Ilemela), Kimochi (Moshi Vijijini).Matokeo zaidi ya rufaa kutoka NEC soma hapa.

"Kikilo (Kondoa), Bereko (Kondoa), Isanga (Maswa Magharibi), Kirumba (Ilemela), Liwale Mjini (Liwale), Mshewe (Mbeya Vijijini), Nar (Babati Vijijini), Namiungo (Tunduru Kaskazini), Kimbiji (Kigamboni), Chitete (Ileje), Dunda (Bagamoyo), Kimambi (Liwale), Ludewa (Ludewa), Mwabusalu (Kisesa), Konje (Handeni Mjini) na Makurumla (Ubungo).

"Tume imekataa rufaa 12 za wagombea udiwani ambao hawakuteuliwa. Rufaa hizo ni kutoka kweye kata za Mwayaya (Buhigwe),Bwakira Chini (Morogoro Kusini),Lalago (Maswa Mashariki), Duga (Tanga Mjini), Makurumla (Ubungo), Ngoywa (Sikonge), Isyesye (Mbeya Mjini), Iwambi (Mbeya Mjini), Oltrumet (Arumeru Magharibi), Iyunga (Mbeya Mjini), Bamilayanga (Mafinga Mjini) na Kahangara (Magu).

Aidha, amesema tume hiyo imekata rufaa tisa za kupinga wagombea udiwani walioteuliwa. Rufaa hizo ni kutoka kwenye kata za Maendeleo (Mbeya Mjini), Forest (Mbeya Mjini), Kashaulili (Mpanda Mjini), Isanga (Mbeya Mjini),Mbalizi Road (Mbeya Mjini), Itende (Mbeya Mjini), Sinde (Mbeya Mjini), Boma (Mafinga Mjini) na Makuro (Singida Kaskazini).Habari mpya soma hapa.

Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi NEC amesema kuwa, idadi hii inafanya jumla ya rufaa za wagombea ubunge zilizofanyiwa uamuzi na tume kufikia 117 na za wagombea udiwani 195.

"Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku.Wahusika wa rufaa watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa tume,"amesema Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt.Wilson Mahera Charles.



Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news