BREAKING NEWS:Daktari,mtaalamu wa dawa za usingizi washikiliwa kwa rushwa

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Kiteto Mkoa wa Manyara inamshikilia, Dkt.Martin John Jongora wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto kwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007, anaripoti MWANDISHI WETU kutoka DIRAMAKINI.

Mwingine anayeshikiliwa kwa tuhuma hizo ni mtaalam wa dawa za usingizi wa hospitali hiyo, Fabiano Aweda. 

 Hayo yamebainishwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Holle Makungu wakati akielezea juu ya hatua hiyo mkoani humo.

Wawili hao wanatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya shilingi 180,000 toka kwa mzee wa miaka sitini aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tezi dume na waliomba rushwa hiyo ili waweze kumfanyia upasuaji licha ya mzee huyo kuwa na Bima ya Afya.

TAKUKURU  Wilaya ya Kiteto ilipokea malalamiko hayo, "tukamuelekeza mlalamikaji aende akawaombe wamfanyie upasuaji kwa kuwa ana bima ya afya, lakini watuhumiwa hao walikataa na kumwambia kuwa, endapo ataendelea kubisha wataandika taarifa kuwa, ugonjwa huo hawawezi kuutibu na watamwandikia rufaa ya kwenda Dodoma ambapo angeingia gharama kubwa zaidi ya usafiri na malazi.

Mkuu huyo amesema kuwa, kwa kuzingatia kuwa Kongora alikuwa mtaalamu pekee katika hospitali hiyo kwa tatizo hilo na hali ya mgonjwa iliendelea kwa mbaya, "tulielekeza rushwa hiyo wapewe wataalamu hao wa afya wakati ushaidi wa kuomba kupkea rushwa ukiendelea kukusanywa.

"Tuliacha wamfanyie mgonjwa upasuaji ambapo walifanya upasuaji huo kwa ufanisi. Vile vile tulisubiri pia mgonjwa huyo apone na kuruhusiwa kutoka hospitali ndipo tuliwakamata. Watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu Septemba 14, 2020. Zinazofanana soma hapa.

"Takukuru Mkoa wa Manyara tunakemea kwa nguvu zote watumishi wachache wa Wizara ya Afya wakaokiuka maadili ya taaluma yao na kujihusisha na vitendo vya rushwa. Tutaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa watumishi wa aina hiyo. Ni rai yangu kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa bila woga kwa kuwa Sheria ya Kuzuia na Kupamba na na Rushwa namba 11/2007 ina vifungu vinavyowalinda watoa taarifa kwa nia njema,"amesema Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Holle Makungu.

.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news