BREAKING NEWS:NEC YATOA UAMUZI WA RUFAA 60 ZA WAGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI

 *Idadi hii inafanya jumla ya rufaa za wagombea ubunge zilizofanyiwa uamuzi na NEC kufikia 113 na za wagombea udiwani 103

"Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha jana tarehe 10 Septemba, 2020 imepitia, imechambua na kuzifanyia uamuzi rufaa za wagombea Ubunge na Udiwani zilizowasilishwa na wagombea kupitia kwa wasimamizi wa uchaguzi nchi nzima.

"Rufaa hizo zimewasilishwa chini ya kifungu cha 40 (6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 kikisomwa pamoja na kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ambacho kinatoa fursa kwa wagombea wa Ubunge na Udiwani kukata rufaa wanapokuwa hawajaridhika na uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi kutokana na pingamizi zilizowasilishwa;

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles akitoa taarifa kwa Umma kuhusu zoezi la kupitia na kufanya uamuzi wa rufaa za wagombea Udiwani na Ubunge leo Septemba 11, 2020 jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 11, 2020 na Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Wilson Mahera Charles ikiwa ni utaratibu wake wa kutoa taarifa kwa umma kila tume inapokamilisha taratibu za kupitia na kuchambua rufaa mbalimbali za wagombea.

Dkt.Charles amesema, katika kikao hicho, tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi jumla ya rufaa 60 kati ya hizo rufaa mbili ni za wagombea ubunge na 58 ni za wagombea udiwani. "Matokeo ya rufaa za wagombea ubunge ni kama ifuatavyo;

"Tume imekubali rufaa moja na kumrejesha mgombea katika orodha ya wagombea. Rufaa hiyo ni kutoka kwenye Jimbo la Iramba Magharibi. Tume imekataa rufaa moja ya mgombea ambaye uteuzi wake ulitenguliwa, rufaa hiyo ni kutoka Jimbo la Iramba Magharibi.

"Aidha, tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 58 za madiwani kama ifuatavyo; imekubali rufaa 34 na kuwarejesha wagombea katika orodha ya wagombea udiwani. Rufaa hizo ni kutoka kwenye kata za Kahororo (Bukoba), Ishozi (Nkenge), Chongoleani (Tanga Jiji), Kirare (Tanga Jiji), Mwamanga (Magu), Ng'haya (Magu).

"Nyingine ni Riroda (Babati Vijijini), Maswa Magharibi (Maswa), Kirumba (Ilemela), Bonga (Babati Vijijini), Kamagambo (Karagwe), Namelock (Kiteto), Masewa (Bariadi), Bweranyange (Karagwe), Kituntu (Karagwe),Kamagambo (Karagwe), Msowero (Kilosa), Lubugu (Magu), Lingeta (Meatu).

"Pia ipo Ifakara (Kilombero), Kiloli (Sikonge), Mkoma (Rorya), Nyamhongolo (Ilemela), Sikonge (Sikonge), Tanganyika (Muheza), Uhenga (Wanging'ombe), Babati (Babati), Vwawa (Mbozi), Lukanga (Mkuranga), Langai (Simanjiro), Lutale (Magu), Majohe (Ilala), Namabengo (Namtumbo) Viwanja Sitini (Kilombero),"amefafanua Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dkt.Charles.Rufaa zilizopita soma hapa.

Aidha, amesema tume imekataa rufaa 23 za wagombea ambao hawakuteuliwa. Rufaa hizo ni kutoka kwenye kata za Ilemela (Ilemela), Kayanze (Mwanza Jiji), Kiarare (Tanga Jiji), Mabawa (Tanga Jiji), Kadoto (Maswa Magharibi), Iyela (Mbeya Jiji), Kirua Vunjo Magharibi (Vunjo), Mji Mpya (Morogoro Mjini).

"Pia ipo rufaa ya Pugu (Ukonga), Tembela (Mbeya Mjini), Vikumburu (Kisarawe), Mecco (Ilemela), Kibara (Mwibara), Kiloleli (Sikonge), Changarawe (Mafinga Mji), Igawilo (Mbeya Mjini), Msonga (Mkuranga), Uru Kaskazini (Moshi Vijijini), Kivukoni (Ilala), Manga (Mbeya Mjini), Nsalaga (Mbeya Mjini) na Jangwani (Ilala)," amebainisha Dkt.Charles.

Amesema, pia tume imekataa rufaa moja ya kupinga walioteuliwa, rufaa hiyo ni kutoka Kata ya Arri (Babati Vijijini).

Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi NEC amesema, idadi hii inafanya jumla ya rufaa za wagombea ubunge zilizofanyiwa uamuzi na tume kufikia 113 na za wagombea udiwani 103. Matokeo ya rufaa zaidi soma hapa.

"Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku. Wahusika wa rufaa hizo watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa tume,"amebainisha Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Wilson Mahera Charles. Mwendelezo wa matokeo ya rufaa za NEC soma hapa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. Diramakini hamlali? Anyway hongereni sana kwa uharaka na umakini wenu. Kazi nzuri

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news