CCM waomboleza kifo cha Jaji Mark Bomani

Katika hatua nyingine, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.Mwigulu Nchemba amesema kuwa kifo cha Jaji Mstaafu Mark Bomani ni pigo kubwa kwa sekta ya sheria na kwamba watahakikisha wanamuenzi kwa kutekeleza yale yote aliyoyaishi na kuyaanzisha.

 Dkt.Nchemba ametoa kauli hiyo leo Septemba 11, 2020 muda mfupi tu tangu taarifa za kifo cha mzee Bomani zianze kusambaa mitandaoni huku akieleza kuwa Jaji huyo alikuwa akisisitiza kwamba sheria zinatungwa ili zitekelezwe.

"Jaji Bomani mara zote alikuwa anasisistiza kwamba sheria zinatungwa ili zitekelezwe, hivyo ni jambo ambalo tutalazimika kama sehemu ya kumuenzi ni kuyaishi kutekeleza zile sheria mabzo alizianzisha na kuzifanyia kazi hadi kufikia hatua ya kutumika,"amesema Dkt.Chemba.

Jaji Mstaafu Mark Bomani amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Septemba 11, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Jaji Bomani alizaliwa Oktoba 22 mwaka 1943, huko Wete visiwani Pemba jijini Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news