Dondoo za kandarasi za soka barani Ulaya Septemba 17,2020

Ni  vya wazi  kuwa,  vilabu vya soka barani Ulaya vina jambo lao, wengine wanakana kukatiza kandarasi, wengine wanaendelea kumwaga wino. 

Ipo hivi, Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amekana ripoti kuwa mchezaji wa nafasi ya kiungo wa kati,Memphis Depay, aliyekuwa akichezea Manchester United, yuko njiani kujiunga na Barcelona. 

Hayo ni kwa mujibu wa Evening Standard huku Sheffield United ikiwa imemfuatilia mshambuliji wa Arsenal,Folarin Balogun.
(Getty Images).

Kwa mujibu waYorkshire Post tayari kocha, Chris Wilder amethibitisha kuhusu mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19.

Huku na kule,RB Leipzig imetishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Leeds United kutokana na kushindwa kumsajili mshambuliaji, Mfaransa Jean-Kevin Augustin.

Kwa mujibu wa Independent, Leipzig imedai kuwa Leeds kulingana na mkataba ilikuwa inatakiwa kumsajili Augustin.

Mshambuliaji huyo alikuwa akicheza kwa mkopo katika klabu ya Elland Road msimu uliopita, kwa kitita cha Pauni milioni 17.7.

Tukirejea, Real Madrid ni kwamba mlinzi wake wa kushoto, Sergio Reguilon miaka 23 yupo katika kiwanja cha mazoezi cha Tottenham kwa vipimo vya afya kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya ligi kuu.

Mhispania huyo anaendelea kufanya hivyo, hii ikiwa ni kwa mujibu wa Evening Standard.

Times  imebainisha kuwa, kocha wa Everton Carlo Ancelotti anataka kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Chelsea Fikayo Tomori.

Aidha yuko tayari kuwaachia wachezaji kadhaa akiwemo viungo wa kati Gylfi Sigurdsson umri wa miaka 31  na Fabian Delph miaka 30 ili kufanikisha kandarasi ya Tomori mwenye miaka 22.

Wakati huo huo, Manchester City wanajiandaa kuwa na uhamisho wa mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga Atletico Madrid, Jose Gimenez.

Kwa mujibu wa Guardian hayo yatajiri ikiwa Napoli itakataa kushusha dau kwa ajili ya mlinzi wa kati Kalidou Koulibaly miaka 29 ili kuweka mambo sawa.

Nao Football.London wanaripoti kuwa,
kiungo mkabaji wa Atletico Madrid Thomas Partey miaka 27 ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Arsenal ingawa akini klabu hiyo ya Uhispania watamuuza iwapo dau la pauni milioni 45 litafikiwa ili waangalie ustaarabu mwingine.

No comments

Powered by Blogger.