Kamanda Mambosasa ajibu madai ya ACT-Wazalendo

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema hafahamu lolote kuhusiana na madai ya kukamatwa kwa maafisa kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Picha. (Mtandao).

SACP Mambosasa amesema hayo leo Septemba 27, 2020 wakati akizungumza na EATV/Radio Digital baada kituo hicho kutaka kufahamu kuhusiana na madai hayo yaliyotolewa na Chama cha ACT-Wazalendo. “Mimi sijui, wala sijapata taarifa zao,"amesema Kamanda huyo kwa ufupi.

Wanaodaiwa kushikiliwa polisi kwa mujibu wa taarifa ya ACT-Wazalendo ni Dahlia Majid (Afisa wa Uchaguzi), Dotto Rangimoto (Afisa Habari Msaidizi) na Arodia Peter (Afisa Habari Uenezi).

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Chama cha ACT-Wazalendo Septemba 25, 2020 na Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe ilielezea juu ya madai ya kushikiliwa kwa maafisa wa kampeni wa chama hicho jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.