KILIMANJARO WAIMARISHA HALI YA ULINZI KATIKA KIPINDI HIKI CHA KAMPENI

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro,Dkt. Anna Mghwira amewataka wanasiasa kutumia majukwaa yao ya kisiasa kutoa matamko ya matumaini kwa wananchi ili kuisadia nchi isonge mbele zaidi badala ya kutumia majukwaa hayo kutoa lugha za matusi.

Akizungumza na Amsha Amsha ya Uhuru FM 2020 nyumbani kwake amesema, kipindi hiki kikitumiwa vizuri na wanasiasa kinasaidia kuwaweka wananchi pamoja,lakini kikitumika vibaya kinaleta mfarakano na vurugu.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akifanya mahojiano na mtangazaji wa Uhuru FM, Emanuel Barnabas nyumbani kwake mjini Moshi.

“Jukumu la wanasiasa kipindi hiki ni kuwaambia wananchi wataongeza thamani gani katika mambo yanayowagusa,maana vitu tayari vipo kinachotakiwa sasa ni kuboresha na kukarabati,”amesema.

Amsema, dhamira ya serikali mkoa ni kuhakikisha Uchaguzi wa Oktoba 28 unafanyika kwa amani na utulivu na kusisitiza kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vipo imara kuhakikisha amani inakuwepo kabla na baada ya uchaguzi.

Ameongeza kuwa, hali ya usalama kwa sasa ni nzuri na hakuna vitisho vyovyote na kusisitiza kuwa wamejiandaa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu na kwamba hadi sasa hakuna vitisho vyovyote vya uvunjifu wa amani.

“Matamanio ya wanasiasa ya jukwaani yatafsirike kwenye maeneo watakayokuwa wanayaongoza, watambue kuwa hawaji kuongoza watu wapya bali ni watu wale wale waliokuwepo,”ameongeza.

Akizungumzia kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwenye mkoa huo kupitia uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano amesema kiasi cha sh.Bilioni 40.3 kimetumika kwa ajili ya kugharamia elimu bila malipo mkoani humo.

Pia zaidi ya sh.Bilioni 43 zimetumika katika ukarabati wa miundombinu katika shule.

“Upande wa miundombinu ya barabara kiasi cha 17sh.Bilioni kimetolewa kwa ajili ya ukarabati wa barabara,ujenzi wa hospitali mpya ya Rombo na Siha na sh. Bilioni 12 kimetumika kukarabati pia jengo la mama na mtoto,”ameongeza.

Mkuu huyo wa mkoa amesema pia wanafuatilia viwanda ambavyo havijaendelezwa mkoani humo na kusisitiza kuwa mali za watanzania zitarudi kwa watanzania.

Akielezea upande wa sekta ya maji amesema kiasi cha sh.bilioni 18 zimetumika katika kuhakikisha wananchi wanapata maji.

“Upande wa mifugo na kilimo tuna mpango wa kuwachimbia visima wafugaji ili mifugo yao ipate maji,ukiangalia wilaya ya Mwanga ndio inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wafugaji,hivyo maji ni muhimu kwao,”amesema.

Wakati huo huo, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi, Jonathan Mabihya amesema, ushindi wa chama hicho kwa mkoa huo mwaka huu ni zaidi ya asilimia 99 kutokana na wananchi kuielewa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ilivyofanya maajabu makubwa kwa kipindi kifupi tu.
Akizungumza na Amsha Amsha ya Uhuru FM Mjini Moshi, Katibu huyo wa CCM mkoa amesema, imani ya ushindi huo inatokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.

Kutokana na hali hiyo amewaomba wananchi kujitokeza katika mikutano ya kampeni ya CCM na hatimaye siku ya Jumatano ya tarehe 28 Oktoba kunipigia Kura za ndio CCM.

Miongoni mwa miradi inayoipaisha CCM katika ushindi wa mwaka huu amesema ni sera ya elimu bure, afya kwa kuboresha na kukarabati Hospitali ya Mawenzi ya Mkoa wa Kilimanjaro, miundombinu pamoja na mradi wa maji ya Mwanga, Same na Korogwe ambayo wananchi wameikubali na kuipongeza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news