Kim Jong-un asema wao ni wakosaji,aiomba msamaha Korea Kusini

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un ameomba msamaha kufuatia mauaji ya afisa wa Korea Kusini.

"Komredi Kim Jong-un na Tume ya Maadili hapa kwa moyo wa unyenyekevu, sisi ni wakosaji, tunaomba msamaha wa haya yaliyojitokeza, tumewakosea, tunaomba msamaha," hayo ni kwa mujibu wa maelezo yaliyonukuliwa kutoka Jamhuri ya Watu wa Korea.
Kufuatia tukio hilo la Ijumaa, Kim ameripotiwa kumwambia mwenzake wa Korea Kusini Moon Jae-in kwamba, tukio hilo halikustahili kufanyika, hivyo wanaomba msamaha.

Korea Kusini inadai mtu huyo mwenye umri wa miaka 47 alikuwa akijaribu kutoroka kutoka Korea Kaskazini alipopatikana na wanajeshi wa nchi hiyo ambao walikuwa wakishika doria ambapo alipigwa risasi na mwili wake kuteketezwa moto.

Hayo yanajiri wakati mpaka kati ya Korea hizo mbili unalindwa vikali na Kaskazini inadaiwa kutekeleza sera ya kuua kwa kupiga risasi ili kumzuia mtu huyo asiingize virusi vya corona (COVID-19) nchini humo.

Msamaha huo ulitolewa kupitia njia ya barua iliyotumiwa Rais Moon kuelezea kuwa tukio hilo halikustahili kufanyika, kwa mujibu wa afisa mmoja nchini humo.

No comments

Powered by Blogger.