KMC FC kucheza na Kagera Sugar kesho Kaitaba

Vinara wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, KMC FC, kesho watashuka dimbani kukutana na Kagera Sugar mchezo utakaopigwa katika Dimba la Kaitaba mkoani Kagera saa nane kamili mchana,anaripoti Christina Mwagala,KMC FC.




Hadi sasa kikosi hicho cha KMC FC ambacho kimeweka kambi mkoani Kagera kipo kwenye uimara wa kutosha na kwamba katika mchezo huo watahakikisha kuwa wanaondoka na ushindi wa alama tatu muhimu ambazo zitawawezesha kuendelea kusalia katika nafasi ya kwanza.

KMC FC inakwenda kucheza mchezo wake wa nne, lakini pia ni wapili ugenini na kwamba hadi sasa haijapoteza mchezo wowote tangu kuanza kwa ligi kuu Tanzania Bara Septemba 17 mwaka huu na hivyo kuiwezesha timu hiyo kuwa na alama tisa pamoja na magoli nane.

Hadi sasa KMC imeshacheza michezo yake ambayo ni dhidi ya Mbeya City, Tanzania Prisons , Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news