KMC FC YAENDELEA KUTAKATA LIGI KUU TANZANIA BARA

TIMU ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC imeendelea kutaka katika msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika msimu wa 2020, 2021 baada ya kuwatunishia misuli timu ya Tanzania Prisons na kuwafunga magoli mawili kwa moja,anaripoti CHRISTINA MWANGALA kutoka KMC FC.

Kwa matokeo hayo imeiwezesha KMC FC hivi sasa kuendelea kuongoza ligi ikiwa na magoli sita pamoja na alama sita jambo ambalo hakuna timu iliyofikisha alama, magoli hayo tangu kuanza kwa msimu huo wa ligi mwaka huu.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa kuvutia na burudani ya aina yake umeiweka KMC FC katika rekodi ya kutopoteza michezo miwili mfululizo tangu kuanza kwa msimu huo wa ligi kuu Tanzania Tanzania Bara 2020 hadi 2021.

Itakumbukwa kuwa Septemba Saba mwaka huu, timu hiyo ilishuka katika dimba la Uhuru na kufanikiwa kuwafunga Mbeya City magoli manne kwa nunge na hivyo kuwa timu ya kwanza kufunga magoli mengi katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu.

Kufuatia matokeo hayo, kikosi hicho cha KMC FC kimeonesha kuwa na kikosi kizuri katika msimu huu na hivyo kutoa taswira ya kuendelea kufanya vizuri katika mechi zijazo ambapo Septemba 21 itakwenda kukutana na timu ya Mwadui ya Mkoani Shinyanga.

Magoli ya KMC FC yamefungwa na Hassan Kabunda mnano dakika ya sita ya mchezo,huku la pilli likifungwa na Kenenth Masumbuko na hivyo kuamsha mashabiki wa timu hiyo ambao jana walijitokeza kwa wingi katika mchezo huo.

No comments

Powered by Blogger.