Lissu awapa 'presha vigogo' waliojimilikisha ardhi kubwa

MGOMBEA Urais kupitia Chama cha Demokrsaia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema iwapo wananchi watampaa ridhaa Oktoba 28, mwaka huu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atahakikisha anakula sahani moja na vigogo waliopora au kujimilikisha ardhi kinyume na taratibu.

"Ni jambo la kushangaza kwamba, maelfu ya hekari ya mashamba yamekaa bure eti kwa sababu wakubwa wameyachukua huku wananchi wanahangaika na hawana pa kulima, kuna vigogo wengi wamejimilikisha ardhi hapa,jambo hili nitalifanyia kazi;

Tundu Lissu aliyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi wa Ifakara katika mwendelezo wa kampeni zake za kuomba kura kuelekea Oktoba 28, mwaka huu.

Mgombea huyo pia amewaombea kura wagombea udiwani na ubunge wa CHADEMA ili wakashirikiane naye kutatua kero za namna hiyo pamoja na kuharakisha maendeleo.

Amesema, iwapo akifanikiwa kushinda nafasi hiyo atahakikisha mashamba yote ambayo yanamilikiwa kinyume na vigogo yanarejeshwa kwa wananchi ili waweze kuyatumia kwa ajili ya kuzalisha. 

Amesema, Morogoro ni sehemu muhimu kwa uchumi wa Taifa kwa kuwa, mazao ya aina mbalimbali ikiwemo miwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari inastawi kwa wingi na hakuna zao linalokataa kustawi mkoani humo

No comments

Powered by Blogger.