Humphrey Polepole:CCM tuna mtaji mkubwa wa kutuwezesha kuibuka kidedea Oktoba 28

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole akisisitza jambo katika mkutano huo. 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema ndani ya miaka mitano chama hicho kimeweza kuwa na ngome ya kuweza kushinda Uchaguzi Mkuu wa 2020 bila ubishi wowote.

Amesema, mtaji mkubwa wa kuibuka kidedea kwenye uchaguzi uliopo mbele yao, ni hazina ya wanachama wanaofikia milioni 17. Hayo ameyasema mjini Chato mkoani Geita wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Polepole akizungumzia kuhusu diplomasia amesema, Serikali ya Awanu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli imeweza kuimarisha uhusiano na mataifa mbalimbali.Zinazouwiana unaweza kusoma hapa.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Humphrey Polepole akiongea na wanahabari mjini Chato mkoa wa Geita, leo Ijumaa Septemba 11, 2020.

Amesema, Serikali imefanikiwa kuimarisha Diplomasia ya Uchumi na Siasa, ikiwemo kufungua Balozi kwenye nchi zingine ili kukuza ushirikiano.
 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news