Lissu atumia muda mwingi kubishana na NEC,muda wa kunadi ilani, sera wakosekana

Tundu Lissu amesema hawezi kwenda jijini Dodoma kuitikia wito wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhudhuria Kikao cha Kamati ya Maadili ya Taifa ya Uchaguzi hadi atakapokabidhiwa malalamiko kama inavyoelekezwa na kanuni na yeye kuyajibu, "na yaletwe moja kwa moja kwangu"., anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mgombea huyo wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrsania na Maendeleo (CHADEMA) amesema,hadi sasa hajapata malalamiko yoyote kama taratibu zinavyoelekeza na yeye kuwasilisha utetezi wake kadri itakavyohitajika.Ameyasema hayo leo jioni Septemba 28,200 mjini Mugumu, Serengeti mkoani Mara wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni.

 Mgombea huyo ambaye ametakiwa mbele ya Kamati ya Maadili ya Taifa ya NEC kesho Septemba 29,mwaka huu amewataka wanachama na wananchi kutokuwa na wasiwasi.

Amedai,hadi sasa hajapelekewa malalamiko yoyote na wala hajaambiwa kama kuna malalamiko hayo na yamepelekwa kwao na mgombea gani, au chama gani cha siasa au kama ni tume yenyewe.

Tundu Lissu amedai, maadili hayo yametengeneza na tume na yanaeleza namna ya kuwasilisha malalamiko yanayokiuka maadili ya uchaguzi, yakibainisha wanaoruhusiwa kupeleka malalamiko juu ya ukiukwaji wa maadili ya uchaguzi huku akisema wanaoruhusiwa kupeleka malalamiko ni wagombea, chama cha siasa,tume au Serikali.

Amesema, maadili yanaelekeza kwamba chama kilichosaini maadili hayo kinatakiwa kuwasilisha malalamiko yake kwa maandishi mbele ya Kamati ya Maadili. "Wanatakiwa waniletee malalamiko kwa maandishi, lakini hadi sasa Mkurugenzi wa Uchaguzi hajasema ni nani amelalamika, pia hajaonesha maandishi yoyote ya malalamiko huyo.

"Kwa hiyo hapa nilipo hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa mtu yeyote, kutoka chama chochote, wala mgombea na hata Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa sababu hiyo siwezi kwenda na sitakwenda Dodoma kesho,"amesema Lissu huku akidai kauli ya kumtaka aende Dodoma iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC,Dkt.Charles Mahera ni ya mtandaoni kama zilivyo kauli zingine za mitandaoni, hivyo hatakwenda kwa sababu hakuna malalamiko.

No comments

Powered by Blogger.