Lowassa: Magufuli, mimi sina mashaka juu ya kushinda tena kwa kishindo,huko kwa kina Lissu wameanza kujipambanua sana, maneno mengi, fujo zile, wanaonekana kwenye mamitaa, matv, matv

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwa Monduli kwenye kikao cha Chama Cha Mapinduzi ambapo mwanae, Fred Lowassa anawania jimbo hilo, alipata fursa ya kuongea na kumuelezea Dkt. John Magufuli aliyoyafanya katika vita dhidi ya virusi vya Corona (Covid-19).

Pia kwenye kikao hicho alikuwepo Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda ambaye anaendelea kumuombea kura Dkt.Magufuli na wagombea wa CCM maeneo mbalimbali.

"Mimi sina mashaka juu ya kushinda, mashaka yangu atapita kwa kura ngapi. Huko kwa kina Lissu wameanza kujipambanua sana, maneno mengi, fujo zile, wanaonekana kwenye mamitaa, matv, matv mengine yanatisha tisha lakini tulimwambia Rais wetu usitishike hata kidogo.

"Umma wa watanzania uko nyuma yako na Dunia inajua kwamba kuna mwanaume Tanzania. Nasema hivyo kwa sababu, Australia kama ulisikiliza BBC leo, Rais anajiuzulu, kule Bolivia Rais anajiuzulu yote kwa sababu ya hii kitu, Corona si mchezo.

"Nyinyi mtu wenu tena mtu mweusi ana nguvu za kimitume anakwenda anawaambia Taifa lake, jamani tumuendee Mwenyezi Mungu, tumuombe atusaidie tuondokane na hili janga. Watu wa ajabu, wakasema huyu anababaisha tu. Anababaisha? Imepita wiki mbili, tatu hamna Corona,"amesema.

No comments

Powered by Blogger.