MAJALIWA AFUNGUA MBIO ZA NMB MARATHON NA KUTOA ZAWADI KWA WASHINDI


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angellah Kairuki wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mlimani City jijini Dar es salaam kufungua Mbio za NMB Marathon na kutoa zawadi kwa washindi Septemba 12, 2020. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Abubakar Kunenge na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt. Edwin Mhede. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya sh.milioni 100 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Maseru, (kushoto) wakati alipohitimisha mbio za NMB Marathon kwenye viwanja vya Mlimani City jijini Dar es salaam, Septemba 12, 2020. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Uwekezaji) Angellah Kairuki, wa tatu kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sanlam East Africa, Julius Magabe na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt.Edwin Mhede. Fedha hizo zilizotolewa na Benki ya NMB zitatumika kuwasaidia watoto wenye ugonjwa saratani wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na washindi wa Mbio za NMB Marathon baada ya kuwakabidhi zawadi washindi hao kwenye viwanja vya Mlimani City jijini Dar es salaam, Septemba 12, 2020. Wa nne kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angellah Kairuki , wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge, Wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Maseru. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sanlam East Africa, Julius Magabe na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt. Edwin Mhede.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news