Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aendelea na kampeni Songea



Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi kitabu cha Ilani ya CCM 2020/25 Mbunge Mteule wa Jimbo la Peramiho, Mhe. Jenista Mhagama kwa ajili ya kuinadi kwenye mikutano ya kampeni za CCM baada ya kuwahutubia wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Jimbo la Peramiho katika Uwanja wa Tamasha Peramiho (A) Wilaya ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma leo Septemba 16,2020.

Jimy Sammwel (18) mwanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Mposeni Wilaya ya Songea Vijijini akiwa na picha yenye Sura ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli alipofika kwenye mkutano CCM uliofanyia katika Uwanja wa Tanmasha Peramiho Wilaya ya Songea Vijijini leo Septemba 16,2020.

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi Jimbo la Peramiho mkutano wa kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM katika Uwanja wa Tamasha Peramiho (A) Wilaya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma leo Septemba 16,2020.

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Jimbo la Peramiho wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM katika Uwanja wa Tamasha Peramiho (A) Wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma leo Septemba 16,2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news