Mamia ya wafuasi wa CHADEMA wanusurika kifo

Mamia ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamenusurika kifo kutokana na ajali iliyotokea maeneo ya Nyanda za Juu Kusini.Wanachadema hao kutoka mjini Songea, Ruvuma walikuwa kwenye msafara wa kumsindikiza mgombea ubunge wa chama hicho, Aden Mayala huku wakikadiriwa kuwa ni zaidi ya 250.

Mmoja wa mashuhuda wameieleza Diramakini kuwa, tukio hilo lilitokea baada ya msafara wao kukumbana uso kwa uso na moja wapo ya malori ya mizigo ambalo lilikuwa limebeba mahindi katika eneo la Daraja la Matawe mjini Songea.

Aidha, Mayala amesema, huenda chanzo cha tukio hilo kilisababishwa na dereva wa lori kuongeza kasi, hivyo kuhatarisha usalama wao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa amethibitisha kutokea tukio hilo ingawa hakuna madhara makubwa yaliyotokea kwenye ajali iliyowahusisha wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wanatoka kwenye mkutano wa mgombea Ubunge Jimbo la Songea Mjini.

No comments

Powered by Blogger.