Mgombea Urais Tundu Lissu asema mambo haya atayatekeleza akipewa ridhaa Oktoba 28,2020

 "Nimesema na sera yetu imesema nitatengeneza mahusiano na nchi zote rafiki, hizo mnazoita nchi za kibeberu ndizo mnazitegemea kwa kila kitu, zinafundisha mpaka majeshi yetu," amesema Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu katika mkutano na waandishi wa habari jijiji Mwanza, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mbali na hayo Lissu amesema, sera ya chama chao inasema itatengeneza mahusiano mema na nchi rafiki ili wawekezaji waweze kuja nchini kuwekeza kwa ustawi wa maendeleo ya taifa na wananchi wake.

Lissu amesema, iwapo Watanzania watampa ridhaa Oktoba 28,mwaka huu ataimarisha mahusiano na nchi za Afrika, Ulaya, Marekani, Urusi, China, Japan  na nyinginezo ili kuifanya nchi kustawi kiuchumi.

Pia amesema, Serikali yake itaruhusu uhuru kamili wa vyombo vya habari ambapo vitafanya kazi bila vipingamizi.

Kuhusu suala la mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, Lissu amesema Serikali yake itasimamia riba ya asilimia tatu ya mkopo ambao anapewa mwanafunzi ambapo anatakiwa kuurejesha baada ya kupata ajira kama ilivyokuwa sheria wakati inaanzishwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini.

Amesema, kuhusu masuala ya makazi bora kwa wananchi atahakikisha anadhibiti bomoa bomoa,bei na kodi ya vifaa vya ujenzi.

Pia atafuta sheria zinazobana watu kupata haki na kutunga zile zinazotetea wananchi.

Sambamba na kutenga fedha kwa ajili ya kuwalipa watu fidia pindi wanapokabiliwa na vikwazo kwa madai kuwa rasilimali zipo.

Amesema,Serikali yake inataka vijana wapate hati za kusafiria kwa ajili ya kwenda nje kutafuta maisha na wawekezaji waje nchini kuwekeza ili watu wafanye biashara na watu waweze kusonga mbele kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news