Mwanafunzi amcharaza mapanga mwalimu darasani, Kamanda Daniel Shillah asema yupo mikononi mwao

“Baadhi ya wanafunzi waliwaleta wazazi wao, lakini huyu mwanafunzi kwa utovu wa nidhamu uliopindukia alikuja na upanga akiwa ameuficha kwenye nguo zake na mwalimu alipohoji kwanini haujaja na mzazi, mwanafunzi akachomoa upanga na kumshambulia mwalimu na akawatisha tisha wanafunzi wengine akapata nafasi ya kukimbia, lakini wakamkata na tumemshikilia na atafikishwa mahakamani;

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Daniel Shillah wakati akielezea kuhusiana na mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Mwita Machamo (17) wa Shule ya Sekondari ya Kiagata kutekeleza uovu huo, anaripoti Mwandishi Diramakini.Amesema, mwanafunzi huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mara kwa kumkata na panga mwalimu wake Majogoro John, baada ya mwanafunzi huyo kushindwa kumpeleka mzazi wake shuleni kama alivyoagizwa na mwalimu.

Kamanda Shillah amesema kuwa, tukio hilo lilitokea shuleni hapo majira ya asubuhi wakati mwalimu anakagua wanafunzi watoro, na ndipo mwanafunzi huyo alimgeukia mwalimu wake na kumkata mapanga.

No comments

Powered by Blogger.