Nani anabaki, nani anaendelea Soka la Ulaya Septemba 15,2020

KLABU ya Tottenham huenda wakamsajili mshambuliaji wa Norway, Alexander Sorloth (24).

Sorloth kwa sasa anacheza kwa mkopo kwenye klabu hiyo ya Uturuki akitokea Crystal Palace. 
Luis Suarez
Kwa mujibu wa Independent,Rais Trabzonspor Ahmet Agoglu ameonyesha utayari.

Wakati huo huo,maafisa wa Werder Bremen wamethibitisha kuwa walifuatwa na Aston Villa kwa ajili ya kiungo wa kati Milot Rashica

Kwa mujibu wa Birmingham Mail, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 anahitajika.

Nao Aston Villa kwa mujibu wa Football Insider,
wamempatia mshambuliaji Keinan Davis (22) kandarasi ya miaka mitatu kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi chao.

Aidha,Luis Suarez anatarajiwa kumaliza msimu wake akiwa benchi wakati mkataba wake ukikaribia kumalizika. 

Suarez mwenye umri wa miaka 33 raia wa Uruguay kwa  mujibu wa ESPN ameambiwa na Barcelona atafute klabu mpya wakati akiwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake akiwa kama mshambuliaji.

Mbali na huyo, kiungo wa Chelsea Conor Gallagher mwenye umri wa miaka 20 anatarajiwa kujiunga na West Bromwich Albion kwa mkopo.

Kwa mujibu wa Football.London, kiungo huyo anajiandaa kusaini kandarasi mpya Stamford Bridge.

Mlinda mlango Emi Martinez, 28, anakamilisha mpango wa uhamisho wa thamani ya pauni milioni 20 kwenda Aston Villa baada ya kuchagua kuondoka kwa washika bunduki. (Evening Standard)

Aston Villa iko mbioni kukamilisha mpango wa kumnasa mshambuliaji Bertrand Traore ,25, kutoka Lyon. (Telegraph, subscription required)

No comments

Powered by Blogger.