Nawaf al-Ahmad Al-Sabah aapishwa kuwa Mfalme mpya wa Kuwait

Nawaf al-Ahmad Al-Sabah ambaye ni mrithi wa kiti cha Ufalme wa Kuwait ameapishwa rasmi kama mtawala mpya wa taifa hilo la Ghuba, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Uapisho huo ambao ulifanyika Septemba 30, mwaka huu unatokana na uteuzi wake ambao ulifanyika siku chache baada ya kifo cha kaka yake Amir Sabah al-Ahmad Al-Sabah Septemba 29,mwaka huu.

Baraza la Mawaziri la Kuwait lilimteua Nawaf al-Ahmad Al-Sabah (83) kama mfalme mpya muda mfupi baada ya Sabah kufariki nchini Marekani, ambako alikuwa amelazwa, akiwa na umri wa miaka 91.

Mwili wa marehemu Emir umepangiwa kuwasili nchini Kuwait leo na msiba utahudhuriwa na ndugu tu kwa sababu ya hatua za usalama wa kiafya, kwa mujibu wa familia ya kifalme nchini humo

"Naapa kwa jina la Allah, kuheshimu katiba na sheria za nchi, kulinda uhuru wote, maslahi na mali ya umma na kulinda uhuru na mamlaka ya mipaka ya nchi,"amesema Mfalme huyo mpya Nawaf al-Ahmad Al-Sabah wakati akipishwa na bunge.

Katika hotuba baada ya kula kiapo,Nawaf al-Ahmad Al-Sabah aliomboleza kifo cha mtangulizi wake, akimuelezea kama ishara ya milele, aliyeifanyia mengi nchi yake na watu wake.

"Ameacha urithi uliojaa mafanikio kwa ngazi ya kitaifa, ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu.Taifa letu linakabiliwa na mazingira magumu katika Kanda yenye machafuko, na njia pekee ya kuyamaliza haya na kuyavuka ni umoja na juhudi za pamoja,"amesema Mfalme Nawaf al-Ahmad Al-Sabah.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news