NEC yatoa uamuzi wa rufaa 87 na kuwarejesha wagombea 47 wa madiwani

"Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 14 Septemba 2020 imepitia, imechambua na kuzifanyia uamuzi rufaa za wagombea udiwani zilizowasilishwa na wagombea kupitia kwa wasimamizi mbalimbali wa uchaguzi nchini, inaripoti DIRAMAKINI.

"Rufaa zimewasilishwa chini ya kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ambacho kinatoa fursa kwa wagombea wa udiwani kukata rufaa wanapokuwa hawajaridhika na uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi kutokana na pingamizi zilizowasilishwa.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt.Wilson Mahera Charles.

"Aidha, chini ya kanuni ya kanuni ya 30 (3) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2020, tume inaweza kukubali au kukataa rufa hizo;

Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dkt.Wilson Mahera Charles ameyasema hayo leo Septemba 15, 2020 wakati akisoma matokeo ya rufaa hizo.

Amesema, katika kikao hicho, tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi jumla ya rufaa 87 za wagombea udiwani,

"Ni kama ifuatavyo, tume imekubali rufaa 47 na kuwarejesha wagombea udiwani katika orodha ya wagombea. Rufaa hizo ni kutoka kwenye kata za Mwanhuzi (Meatu), Kondoa (Kondoa Mjini), Isuto (Mbeya Vijijini), Msasa (Handeni Mjini), Bunju (Kawe), Bunju (Kawe), Ipagala (Dodoma Mjini),Iwiji (Mbeya Vijijini), Kichangani (Morogoro Mjini), 

"Kimara (Ubungo), Likongowele (Liwale), Matumbulu (Dodoma Mjini), Nsalala (Mbeya Vijijini), Ulenje (Mbeya Vijijini), Muriti (Ukerewe), Ruvu (Same Magharibi), Kisutu (Bagamoyo), Majimaji (Tunduru), Mtibwa (Mvomero), Unyianga (Singida Mjini na Kagondo (Bukoba Mjini).

"Nyingine ni Kaloleni (Moshi Mjini), Mlabani (Kilombero), Fukayosi (Bagamoyo), Igurwa (Karagwe), Kauzeni (Morogoro Mjini), Maisaka (Babati Mjini), Ndama (Karagwe), Olorien/Magaiduru (Ngorongoro), Kilole (Lushoto), Ngwelo (Lushoto), Hondomairo (Kondoa Mjini).

"Pia kuna Nyasiura (Bunda Mjini), Ikhanoda (Singida Kaskazini), Nyabiyonza (Karagwe),Kibiti (Kibiti), Ruvu Remit (Simanjiro), Ihanda (Karagwe), Mabanda (Handeni Mjini), Bungu (Kibiti), Kapala Msenga (Mpanda Vijijini), Businde (Kyerwa), Igoma (Mbeya Vijijini), Likongowele (Liwale), Shizuvi (Mbeya Vijijini), Mlembwe (Liwale), na Tambukareli (Dodoma Mjini).

Wakati huo huo, Dkt.Charles amesema kuwa, tume imekataa rufaa 30 za wagombea udiwani ambao hawakuteuliwa. Rufaa hizo ni kutoka kwenye kata za Tongwe (Muheza), Kiomboi (Iramba Magharibi), Jangwani (Ilala), Mlali (Mvomero), Kiloleni (Sikonge), Mbasa (Kilombero), Dakawa (Mvomero), Dakawa (Mvomero), Jibondo (Mafia), Kigombe (Muheza).

"Nyingine ni Buhumbi ( Magu), Mlali (Mvomero), Olbalbal (Ngorongoro), Kidete (Kilosa), Bugene (Karagwe), Kihanga (Karagwe), Mabogini (Moshi Vijijini), Hemtoye (Mlalo), Mlali (Mvomero), Mbaramo (Mlalo), Mbaru (Mlalo), Okaoni (Moshi Vijijini), Nangando (Liwale), Magomeni (Kinondoni), Kitangiri (Ilemela), Dareda (Babati Vijijini), Iganjo (Mbeya Mjini), Ipembe (Singida Mjini), Kilema Kaskazini (Vunjo) na Nyamhongolo (Ilemela).

Dkt.Charles amesema, pia tume imekataa rufaa 10 za kupinga matokeo ya udiwani walioteuliwa. Rufaa hizo ni kutoka kwenye kata za Forest (Mbeya Mjini), Mabatini ( Mbeya Mjini), Mkowe (Kalambo), Kaloleni (Moshi Mjini), Mwangoi (Mlalo), Malibwi (Lushoto). Kwa Kilosa (Iringa Mjini),Kihesa (Iringa Mjini),Nzubuka (Tabora Kaskazini), na Ihumwa (Dodoma Mjini).

"Idadi hii inafanya jumla ya rufaa za wagombea udiwani zilizolewa uamuzi kufikia 331. Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku.. Wahusika wa rufaa hizo watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa tume,"amesema Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt.Wilson Mahera Charles.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news