NEC:Tupo huru kweli kweli na tunasimamia uchaguzi huru na haki kwa wagombea wa vyama vyote nchini

MKURUGENZI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Dkt. Wilson Mahera Charles amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni huru kwa kuwa inafanya kazi kwa mujibu wa sheria na si kwa presha ya vyama vya siasa,anaripoti RACHEL BALAMA (Diramakini) DAR ES SALAAM.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa Tume na Watoa huduma ya Habari Mitandaoni katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) leo Septemba 15, 2020 jijini Dar es Salaam.
Amesema,NEC inasimamia uchaguzi ulio huru na haki kwa kutoa nafasi sawa kwa vyama vyote.

Dkt. Mahera ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo Septemba 15,2020 katika mkutano na watoa huduma ya habari za mitandaoni uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Amesema, tume huru ni ile yenye watendaji watanzania wanaozingatia sheria na kwamba tume huru haiwezi kuongozwa na watu kutoka nje ya nchi eti ndo iwe huru. 

Amesema,Ibara ya 74 kufungu kidogo cha cha 7,11 na cha 14 kinasema tume itakuwa huru kwa kufanya kazi bila kuingiliwa na mtu au chama chochote.

Amesema, tume imekuwa ikiwashirikisha watu kutoka vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi kwenye kamati mbalimbali zinazoundwa na tume. 

Dkt. Mahera amewataka watanzania kuwachagua viongozi watakaowaletea maendeleo na si watakaoleta mitafaruku nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news