Prof. Lipumba: Bakora za CCM hazina ubaguzi, tupeni nafasi mfurahi

"Tunaomba kura zenu ili biashara zitoke na wananchi waweze kufanya biashara, uwekezaji uongezeke, vitunguu vipate soko sio tu Tanzania mpaka Afrika Mashariki yote, watu wapewe utaalamu wa kuweza kuongeza tija katika shughuli zao za kilimo.
Mgombea Urais kupitia CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
"Maana mkiwapa CCM miaka mitano mingine, hivyo vyuma si ndiyo vitatumaliza kabisa, kama hivi sasa vijana wa Ilula mnazeeka kabla ya wakati wenu unaweza ukaja hapa ukamwamkia mtu shikamoo kumbe ni kijana wa juzi bakora za CCM zimemchanganya, kila mtu yupo hoi bin taabani na ndugu zangu bakora za CCM hazina ubaguzi;

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ambaye ni mgombea urais kupitia CUF ameyasema hayo Septemba 13, mwaka huu wakati akiendelea na kampeni zake za kuomba wananchi ifikapo Oktoba 28, mwaka huu wampe kura kwa nafasi ya urais, kuchagua wabunge wa CUF na madiwani ili wakawape furaha.

Ameyasema hayo katika mwendelezo wa kampeni zake mkoani Iringa huku akisisitiza kuwa, CUF ikipewa ridhaa wameazimia kuwekeza katika rasilimali watu, elimu, afya na miradi mbalimbali ambayo itawakwamua wananchi katika umaskini.

Pia amesisitiza kuwa,wakipewa ridhaa watauenzi Muungano uliopo kati ya Tanzania Bara na Zanzibar kwani ni nguzo muhimu kwa Taifa na haki sawa itapewa nafasi kwa pande zote.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa Serikali yake itakipa umuhimu mkubwa kilimo kutokana na faida zake kwa jamii na Taifa, kwani kiunasaidia upatikanaji wa malighafi za viwandani ambazo zina umuhimu mkubwa katika kukuza uchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news