Profesa Lipumba asema akopeshwe kura akalipe maendeleo

Profesa Ibrahim Haruna Lipumba ambaye ni Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi (CUF) ameomba akopeshwe kura Oktoba 28, mwaka huu ili akalipe deni hilo kupitia maendeleo.

Lipumba ambaye ni mbobezi wa masuala ya uchumi pia amewaahidi Wana Ushetu kuwa endapo watamchagua na kuingia madarakani atawakumbuka mapema.

Ameyasema hayo leo Septemba 29,2020 wakati akiwahutubia wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Shinyanga.

Pia amedai licha ya wagombea wao kuenguliwa iwapo atachaguliwa kuwa rais atahakikisha kila mmoja anapata haki sawa bila kubagua mtu yeyote.

Lipumba amesema kuwa, amefika maeneo mbalimbali na ameona adha zinazowakabili wananchi wa wilaya hiyo licha ya wao kutokuwa na mgombea ubunge, endapo watamchagua atahakikisha anawakumbuka katika miundombinu, afya,elimu na maji.

No comments

Powered by Blogger.