Rais Edgar Lungu:Asante binti yangu, umenipa heshima

Septemba 26, 2020 imekuwa siku ya furaha na kumbukumbu kwa familia ya Rais wa Zambia Edgar Lungu baada ya kushuhudia harusi ya aina yake kwa binti yao Tasila Lungu na mumewe Patrick Mwansa, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Ndoa hiyo ilifungwa katika Kanisa Katoliki la St. Ignatius Parish ya Lusaka nchini Zambia na baadae kufuatiwa na sherehe kubwa ambayo ilijumuisha wageni kutoka ndani na nje ya nchi.


"Mmeniheshimisha wananngu ninawaomba mzingatie neno la Mungu kutoka Kitabu cha 1 Wakorintho 13:4-7,
Bibilia Takatifu inasema;
4 Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna wivu au majivuno.

5 Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hautafuti kujipendeza nafsi; haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya. 6 Upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia kweli. 7 Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahim ili yote.Mungu awabariki sana,"Rais Edgar Lungu.

No comments

Powered by Blogger.