Rais Macron amtaka Rais Putin kusema ukweli

RAIS wa Urusi,Vladimir Putin ametakiwa kutoa ufafanuzi wa haraka kuhusu jaribio la mauaji dhidi ya mkosoaji na mpinzani wake, Alexei Navalny.
Ni baada ya uchunguzi kuthibitisha kuwa,Navalny alilishwa sumu hatari ya kemikali ya Novichok.

Wito huo umetolewa na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.

 Kwa mujibu wa Ikulu ya Rais wa Ufaransa Elysee, Rais Macron alimemweleza Rais Putin kwa njia ya simu kwamba ni muhimu aeleze anayoyajua bila kuchelewa kuhusu tukio hilo la jaribio la mauaji ya mwanasiasa huyo.

 Rais Macron pia amemweleza Rais Putin kuwa, uchunguzi wao umethibitisha kama ule uliofanywa na Ujerumani kuwa Navalny alipewa sumu aina ya Novichok.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news