Rais Outtara,Gbagbo,Soro kupimana ubavu

BARAZA la Katiba nchini Ivory Coast limemuidhinisha, Rais Alassane Outtara mwenye umri wa miaka 78 kuwania muhula wa tatu wa urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31,2020.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo pia baraza hilo limepunguza idadi ya wagombea wa urais hadi wanne jambo ambalo linadaiwa kuwa linalenga kubinya demokrasia. 
Rais Alassane Outtara

Ni kutokana na ukweli kwamba,awali wagombea 44 wa urais walikuwa wameidhinishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchuana katika uchaguzi huo akiwemo Rais Ouattara ambaye yuko madarakani tangu mwaka 2010. 

Aidha,Baraza la Katiba la Ivory Coast limemuidhinisha rais wa zamani wa nchi hiyo, Laurent Gbagbo ambaye mwaka jana aliachiwa huru na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) na aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi, Guillaume Soro. 

Viongozi hao wawili hao kwa sasa wanaishi Ughaibuni, lakini wana ushawishi mkubwa na wafuasi wengi ndani ya Taifa hilo la Afrika Magharibi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news