Serikali yatatua changamoto ya uhaba wa maji Longido

Serikali kupitia mradi wa maji wa Longido imewezesha upatikanaji wa maji katika mjii wa Longido na Kijiji cha Engikaret kwa asilimia 100. 

Baada ya kukamilisha utekelezaji wa mradi wenye thamani ya shilingi biloni 14.6 ambao unapokea maji kutoka chanzo cha Mto Simba, na umekamilika mwezi Machi mwaka huu,anaripoti Evaristy Masuha (WM).

Akizungumza na Wataalamu wa Wizara ya Maji waliopo katika ziara ya kukagua na kutathimini maendeleo ya miradi ya maji katika mkoa wa Arusha Mhandisi,Salum Rasul kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi  Arusha  (AUWSA) alisema mradi huo ni mkombozi kwa wakazi wa Longido na kijiji cha Engikareti maeneo ambayo yalikuwa na changamoto ya huduma ya majisafi na salama.

“Mradi ulitekezwa kwa lengo la kuongeza huduma ya maji kutoka asilimia 15  ambayo ilikuwa inawezesha wakazi 2,510 mwaka 2017 hadi asilimia 100 sawa na wakazi 16,712 waliopo sasa katika mji wa Longido. Pamoja na wakazi 1,294  wa kijiji cha Engikaret.

Alisema mradi huo umezingatia taratibu zote za afya. Ikiwemo kuhakikkisha maji hayo hayana madini ya Floride yanayozidi kiwango. Akibainisha kwamba hiyo ni hatua nzuri kwa maendeleo ya wananchi wa Longido na Mkoa wa Arusha kwa ujumla.

Nae mkuu wa msafara wa wataalamu waliotoka Wizara ya Maji,  Ingrid Sanda alisema serikali imejipanga kuhakikisha inamtua mama ndoo ya maji kama ilivyoahidi. Huku akiwataka wakazi wa maeneo hayo kuhakikisha wanailinda miundombinu ya maji ili isiharibike.

Kwa upande wake Anna Revocatus ambae ni mkazi wa Longido alisema maji hayo yamewawezesha kubadili maisha kwa kuanzisha kilimo cha bustani na kuwezesha mazingira yakupendeza.

"Kwa kweli nina miaka kumi hapa. Nimekuwepo wakati mji unapambana na changamoto ya upatikanaji wa maji. Hali ilikuwa Mbaya sana. Nashukuru kukamilika mradi huu wa maji, sasa hivi naweza kufanya kazi zangu kwa uhakika. Nimeweza kulima bustani ya Mbogamboga, matunda, na ninajipanga kuanza kilimo cha kisasa cha bustani kwa kutumia maji haya," Anna alishukuru serikali.

Mwananchi mwingine, Abel Kundaeli alisema ameanzisha shamba la vitunguuu na matarajio yake ni kuuza ndani na nie ya nchi. Akiongeza kusema kwamba kwa sasa shamba hilo limetoa ajira kwa watu kumi na anatarajia kupanua zaidi. 

Kuhusu gharama za maji Abel alisema ni nafuuu sana ukilinganisha na soko la bidhaa za kilimo katika miji ya Arusha na chi jirani ya Kenya. Kwahiyo hana wasiwasi na mapato.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news