TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO NCHINI MISRI KATIKA CHUO KIKUU CHA AL–AZHAR MWAKA WA MASOMO 2020/2021

 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar inatangaza nafasi za masomo zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Al –Azhar nchini Misri katika fani mbalimbali kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza na kuendelea kwa mwaka wa masomo 2020/2021.

Masomo yatadhaminiwa: 

•Gharama za Ada 

•Tiketi ya kwenda na kurudi

•Makaazi na kadhalika.

Muombaji anatakiwa awe: 

•Muislamu.

•Hajawahi kuomba nafasi hii na kuteuliwa kisha akaipoteza kwa sababu yoyote ile.

•Asiwe na maradhi ya kudumu au kuambukiza.

•Asiwe ameteuliwa katika sehemu nyingine ndani ya Misri au kwingineko.

•Jina la muombaji liende sambamba na majina yaliyopo katika vyeti vyake vyote vinavyotakiwa kuambatanishwa.

NJIA YA KUFANYA MAOMBI

Fomu za maombi zinapatikana Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar,katika Kitengo cha Uratibu wa Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia na waombaji wote wanatakiwa kuwasilisha maombi yao chumba namba 57 wakiambatanisha na vitu vifuatavyo:

•Vivuli cha cheti cha kumaliza masomo, vigongwe muhuri wa Mahakama, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa Misri nchini Tanzania.

•“Transcript” za masomo aliyohitimu na kupata vyeti hivyo,vigongwe muhuri wa Mahakama, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa Misri nchini Tanzania.

•Kivuli cha cheti cha kuzaliwa kilichogongwa muhuri wa Mahakama, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa Misri nchini Tanzania.

•Picha sita za paspoti za karibuni nyuma ziandikwe jina lake na utaifa wake.

•Awe na barua ya uthibitisho kutoka katika chuo alichosoma

•Tazkia kutoka katika taasisi zinazokubalika na Serikali.

•Kivuli cha pasi ya kusafiria iliyohalali

•Fomu ya uchunguzi wa afya (Medical Report)Mwisho wa kuwasilisha maombi ni Septemba, 2020.Kwa maelezo zaidi fika chumba No. 57 ghorofa ya pili.

No comments

Powered by Blogger.