Tetesi za soka, watampata Chris Smalling,Sergino Dest?

Klabu za Barcelona na Bayern Munich zimeweka ofa ya kumsajili Mlinzi wa kulia wa Ajax na Marekani, Sergino Dest mwenye umri wa miaka 19. (Marca)

Bayern imewasiliana na Mario Gotze kuhusu kujiunga tena na klabu hiyo. Mshambuliaji huyo wa Ujerumani, 28, ni mchezaji huru baada ya kuondoka Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu uliopita. (Sport Bild - in German).

Nao PSG wanamtaka beki wa Chelsea Mjerumani Antonio Rudiger, 27, kwa mkopo wa msimu mzima. (Mail)

Roma wanatarajiwa kuweka ofa nyingine ya pili kwa ajili ya mlinzi wa Manchester United na England Chris Smalling mwenye umri wa miaka 30, ambaye aliichezea timu hiyo ya ligi ya Serie A kwa mkopo msimu uliopita. (Guardian).
Chris Smalling.(Soccrates Images/Getty Images).

Wakati huo huo, mlinzi wa Brazil Alex Telles mwenye umri wa miaka 27 anataka kuondoka klabu ya Porto na kujiunga na Manchester United, ambao wanajaribu kushawishi kupunguziwa dau lake la £36.6m. (Telegraph - subscription required).

Pia Liverpool wanatarajiwa kumtumia mshambuliaji Sadio Mane kumshawishi mchezaji mwenzake wa Kimataifa wa Senegali Kalidou Koulibaly ili atue katika klabu hiyo kutoka Napoli, licha ya Manchester City na Paris St-Germain kuonyesha nia ya kumsaini mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 29. (Le Parisien, via Sun).

Aidha, West Ham wako tayari kupambana na Manchester United kwa ajili ya kupata saini ya beki wa kati wa Swansea City na Wales Joe Rodon mwenye umri wa miaka 22. (Guardian).Wrexham imetengaza ofa kutoka kwa mmiliki mpya nyota wa Hollywood, Ryan Reynolds.

West Ham United imeweka ofa yenye thamani inayofikia £33m kwa ajili ya mlinzi wa kati wa Saint-Etienne Wesley Fofana mwenye umri wa miaka 19 ambaye anawaniwa pia huko Leicester City. (Sky Sports).

Mbali na hayo, Burnley wako kwenye mazungumzo na Liverpool kuhusu kumsajili winga wa wekundu hao na Wales, Harry Wilson mwenye umri wa miaka 23. (Independent)

Huku Lazio ikiwa imefikia makubaliano na Southampton kwa ajili ya mlinzi wa Uholanzi, Wesley Hoedt mwenye umri wa miaka 26 ili kurejea kwenye klabu hiyo ya Italia kwa mkopo. (Sky Sport).

Mlinzi wa kulia wa Atletico Madrid na Colombia Santiago Arias mwenye umri wa miaka 28, amewasili Ujerumani kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na Bayer Leverkusen. (Marca). Naye mshambuliaji wa zamani wa Italia Francesco Totti anatarajiwa kurudi Roma kama mkurugenzi wao mkuu wa michezo. (Corriere dello Sport - in Italian).

Roma wanatarajiwa kuweka ofa nyingine ya pili kwa ajili ya mlinzi wa Manchester United na England Chris Smalling mwenye umri wa miaka 30 huku Atletico Madrid wanalenga kumsajili kiungo wa Arsenal na Uruguay Lucas Torreira mwenye umri wa miaka 23. (Mundo Deportivo - in Spanish).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news