Manchester United itamruhusu winga raia wa Wales Daniel James, kujiunga na Leeds United kwa mkopo, lakini kama watamsajili Sancho hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa Sun. Huku Everton na Leicester City zote zinamnyatia mlinzi wa Chelsea raia wa Ufaransa Kurt Zouma (25) hayo yakiwa ni kwa mujibu wa Talk Sport.
Kurt Zouma. (GettyImages). |
Aidha, Barcelona kwa mujibu wa Goal, inakaribia kufikia makubaliano ya mwisho na Ajax kuhusu beki
wa kulia wa Marekani Sergino Dest (19), lakini ina uwezo mdogo wa kufanya
makubaliano zaidi ya usajili. Cope inaeleza kuwa,mlinzi wa Tottenham na Argentina Juan Foyth (22) ndiye mlengwa wa Valencia.
Leeds United iko katika hatua ya mwisho ya majadiliano na Bayern Munich kuhusu kiungo wa kati Mickael Cuisance (21), baada ya raia huyo wa Ufaransa kuiarifu klabu yake ya Ujerumani kuwa anataka kuingia kwenye kikosi cha wachezaji mara kwa mara, hii ikiwa ni kwa mujibu wa Sport Bible.
Sky Sports wanasema, Lyon ipo tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa, Houssem Aouar (22) ambaye anahusishwa na kuhamia Arsenal.
Kwa upande wa Mail wanaeleza kuwa, kocha wa Everton Carlo Ancelotti hatarajii kuwa winga Theo Walcott (31),ataondoka katika klabu hiyo kipindi hiki cha usajili.
Wakati huo huo, Lazio
inafanya mazungumzo kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United raia
wa Brazil Andreas Pereira (24), kwa kipindi kirefu kwa mkopo kukiwa na
chaguo la kumnunua,Telegraph imeeleza.