Tetesi:Newcastle United, Valencia kupambana kumsajili mlinzi wa Juventus, Daniele Rugani huku Fulham,Sevilla, West Ham wakimyatia

Kwa mujibu wa Express, Klabu ya Arsenal wapo kwenye mazungumzo ya kumtoa kwa mkopo kiungo wao wa kati Matteo Guendouzi kwenda Marseille.Wakati huo huo Star imedokeza kuwa, Klabu ya Chelsea inaweza kuongeza wachezaji kwa kumuuza mlinzi Marcos Alsonso (29), beki wa kati Antonio Rudiger (27),kiungo wa kati Ruben Loftus-Cheek (24) kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Picha na Filippo Alfero-Juventus FC/Juventus FC via Getty Images.

Aidha, Sportitalia imejuza kuwa, Newcastle United wanajiandaa kupambana na Valencia katika mbio za kumsajili mlinzi wa Juventus, Daniele Rugani ambaye pia anahusishwa na taarifa za kutakiwa na Fulham,Sevilla na West Ham.

Sun inaripoti kuwa, Klabu ya Liverpool wanajiandaa kukubali ofa ya pauni milioni 23 kutoka Sheffield kwa ajili ya mshambuliaji Rhian Brewster.

Manchester Evening News wamebainisha kuwa, Manchester United wamekataa kuhusishwa kwao na taarifa za kumsajili Ainsley Maitland-Niles (23) ambaye anaweza kucheza nafasi ya ulinzi na kiungo wa kati kutoka Arsenal.

Aidha, Mirror inaripoti kuwa, Manchester United imeanza mazungumzo na Barcelona kuhusu kumchukua kwa mkopo mshambuliaji Mfaransa Ousmane Dembele (23).

Katika hatua nyingine, Mail inaripoti kuwa, Klabu ya Tottenham wamemaliza makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Benfica, Carlos Vinicius (25) kwa mkopo, ambaye gharama ya kuondoka kwake ni kiasi cha pauni milioni 89 kwa mujibu wa mkataba.

Post a Comment

0 Comments