Thiago Silva:Ninajisikia furaha sana kuwa hapa

Thiago Silva ambaye ni mlinzi wa Chelsea anasema hana wasiwasi na kasi ya Ligi ya Premier licha ya kutimiza miaka 36 siku moja kabla ya kujitokeza katika klabu hiyo.
Mlinzi wa Chelsea, Thiago Silva. (Diramakini).

Beki huyo wa kati wa Brazil aliungana na Frank Lampard wa Blues kwa uhamisho wa bure mwezi uliopita, baada ya kushinda mataji saba ya Ligi akiwa na Paris St.Germain.

Silva atacheza katika mechi ya Jumatano kwenye raundi ya tatu ya Kombe la Carabao wakiwa nyumbani dhidi ya Barnsley."Umri ni namba tu kwenye stakabadhi yako. Sina wasiwasi kabisa kuhusu kasi ya Ligi ya Premier.

"Kimwili, najihisi kijana na nimejitayarisha vilivyo kwa hili. Pia najisikia furaha sana kuwa hapa. Watu wanaonijua, wanafahamu ni kiwango gani ninapenda kazi yangu, vile ninavyojitahidi kuweka nguvu yangu kwa asilimia 200. Hii ni fursa nzuri ambayo Chelsea na Frank Lampard wamenipa na sitaki kuwakatisha tamaa,"amesema.

"Nakuja hapa kama mchezaji mzoefu, na hivyo basi naona vile Chelsea na Frank Lampard wanavyotaka mchezaji mwenye tajriba kama yangu," Silva aliongeza.

No comments

Powered by Blogger.