Tundu Lissu awageukia wafanyabiashara wenye madeni

“Kuwa na deni sio ishu, kama unanilazimisha nilipe deni ili watoto walale njaa kwa sababu tu ya deni hiyo sio sawasawa,kama unataka nilipe deni ili biashara yangu ife hiyo sio sawasawa.
"Kwa hivyo tutaweka utaratibu kwa wafanyabiashara wenye madeni wataweza kulipa madeni yao bila kuua biashara zao;

Hayo yamesemwa na Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Tundu Lissu.

Ameyasema hayo Septemba 14, 2020 katika kampeni zake zilizofanyika katika Mji wa Makambako na kuongeza kuwa atahakikisha wafanyabiashara ambao kweli wana madeni wanawekewa utaratibu mzuri wa kulipa ili wasiathiri biashara zao.

Pia amesema, ataboresha mahusiano ya Kimataifa yenye kuleta tija katika uchumi wa Tanzania endapo Watanzania watampa ridhaa Oktoba 28, mwaka huu.

No comments

Powered by Blogger.