Tundu Lissu mbele ya Kamati ya Maadili

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemuandikia barua mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ya kumuita katika kikao cha Kamati ya Maadili ya Taifa,anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Charles Mahera amesema hayo leo jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa, mgombea huyo atafika mbele ya kamati Septemba 29, mwaka huu.

Akizungumzia utaratibu na usimamizi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,mwaka huu,Dkt.Mahera amesema, tume imekumbana na changamoto kwa baadhi ya wagombea wa kiti cha Rais kutoheshimu sheria, taratibu na maadili ya uchaguzi.

Ameongeza kuwa, baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia maneno ya kukashifu wagombea wenzao, tume, pamoja na kutoa taarifa zisizo za kweli zenye lengo la kuleta taharuki na uzushi miongoni mwa Watanzania.

No comments

Powered by Blogger.