Tundu Lissu:Sitarajii kuacha kampeni ili kuitikia wito wa mitandaoni wa mtu yeyote

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia,Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema hajapokea malalamiko yoyote kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), yanayohusu mwenendo wa ufanyaji wa kampeni zake, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Pia amedai kuwa, hatohudhuria suala lolote linalohusiana na kampeni zake kwa sasa.

Lissu ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, zikiwa zimepita saa kadhaa tu tangu NEC, ilipotoa tamko kwamba, imemuandikia barua mgombea huyo kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kuikashifu NEC kwamba itaiba kura zake.

Sambamba na madai ya kwamba mgombea urais wa CCM, Dkt. Jonh Magufuli atakutana na wakurugenzi wa halmashauri hivi karibuni. Wito wa NEC kwa Lissu upo hapa.

"Sijapokea malalamiko yoyote juu ya jambo lolote linalohusiana na kampeni za uchaguzi mkuu huu kutoka NEC, sijapokea wito wowote kuhusu jambo lolote linalohusiana na kampeni za uchaguzi mkuu huu kutoka NEC, sitarajii kuacha kampeni ili kuitikia wito wa mitandaoni wa mtu yeyote,"amedai Tundu Lissu.

 Septemba 27, 2020, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Charles Mahera, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mkoani Arusha, alisema kuwa Lissu alitoa tuhuma hizo kwenye mikutano yake ya kampeni mjini Musoma kati ya Septemba 25 na 26 mwaka huu, hivyo anatakiwa mbele ya Kamati ya Maadili ya Taifa. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news