Uzinduzi wa nyumba za 'ZSSF Mbweni Real Estate' wafana, Rais Shein awataka wanunuzi kuheshimu sheria za ujenzi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein amewataka wanunuzi wa nyumba katika eneo la mradi wa nyumba za makazi Mbweni, kuheshimu sheria za ujenzi wa nyumba hizo na kuzingatia ramani,anaripoti Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar.

Dkt.Shein ametoa kauli hiyo katika hafla ya ufunguzi wa mradi wa nyumba za maakazi ‘ZSSF Mbweni Real estate’, iliyofanyika eneo la Mbweni, nje kidogo ya Jiji la Zanzibar.

Amesema, kuna umuhimu kwa wanunuzi wa nyumba hizo kuheshimu sheria za ujenzi unaozingatia ramani halisi na hivyo kuepuka hatua zozozte za kuzifanyia mabadiliko ya muundo au kuzipaka rangi, kinyume na taratibu.

Amesema sio jambo la busara kwa wananchi wanaonunua nyumba hizo bila ya kujali ramani halisi ya ujenzi wakaanza kuzifanyia mabadilko kwa kuzingatia kuwa nyumba hizo ni za kisasa, sambamba na kusisitiza matumizi bora na taratibu njema za kuishi , zinazoepusha ufugaji wa aina mbali mbali za mifugo. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dt.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na viongozi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mradi wa Nyumba za Makaazi za "ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ANGENEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuzifungua rasmi Septemba 21, 2020. (IKULU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya ZSSF, Dkt.Suleiman Rashid Mohamed alipowasili katika viwanja vya Mradi wa Nyumba za Makaazi za "ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ANGENEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuzifungua rasmi Septemba 21,2020. (IKULU).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa ZSSF,Sabra Issa Machano alipowasili katika viwanja vya Mradi wa Nyumba za Makaazi za"ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ANGENEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuzifungua rasmi Septemba 21, 2020. (IKULU).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (katikati) wakifuatana na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa ZSSF, Sabra Issa Machano pamoja na viongozi wengine mara baada ya kukagua nyumba za Mradi wa Nyumba za Makaazi za"ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ANGENEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam alipofanya ufunguzi rasmi Septemba 21, 2020. (IKULU).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa ZSSF, Sabra Issa Machano (kushoto) mara baada ya kukagua Nyumba za Mradi wa Nyumba za Makaazi za "ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ANGENEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam alipofanya ufunguzi rasmi leo,kulia ni Waziri wa Fedha na Uchumi, Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa. (IKULU).
Baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria katika Ufunguzi wa Mradi wa Nyumba za Makaazi za "ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ANGENEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam, zilizofunguliwana Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) Septemba 21, 2020. (IKULU).

Viongozi mbalimbali kutoka taasisi za Serikali waliohudhuria katika Ufunguzi wa Mradi wa Nyumba za makaazi za"ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ANGENEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam zilizofunguliwa Septemba 21, 2020 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).(IKULU).

Baadhi ya wafanyakazi wa idara mbalimbali za Mfuko wa ZSSF wakiwa katika hafla ya ufunguzi wa Mradi wa Nyumba za Makaazi za"ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ANGENEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam zilizofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).(IKULU).

“Tuzingatie kwamba nyumba hizi ni za kisasa, tunahitaji tuzitumie kisasa, shughuli kama zile za kutwanga, kufuga kuku na nyenginezo itabidi tuangalie uwezekano wa kuzifanya sehemu nyengine”, alisema.

Amesema nyumba hizo ni za gharama kubwa, hivyo akaitaka ZSSF kuondokana na muhali katika ukusanyaji wa fedha ili hatimae ziweze kulipia gharama za ujenzi.

Amewataka wanunuzi wasighafilike kulipa madeni yao ili ZSSF iweze kupata nguvu na kubuni miradi mingine ya maendeleo.

Dkt.Shein amesitiza umuhimu wa wakazi wa nyumba hizo kuendeleza silka na tamaduni za maisha ya Kizanzibari kwa kuishi kwa ujirani na mashirkiano.

Aidha, Rais Dkt.Shein amesema, ujenzi wa nyumba hizo ni mfano mzuri wa namna Serikali inavyotekeleza dhamira ya matumizi bora ya ardhi iliopo, pamoja na utekelezaji wa vitendo wa azma ya muasisi wa Mapinduzi matukufu ya ya Zanzibar ya 1964, marehemu Abeid Amani Karume katika kuwapatia wananchi makaazi bora, ingawaje wametumia fedha zao.

Amesema, marehemu mzee Karume alianza na ujenzi wa nyumba za kisasa katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba, ikiwemo Kikwajuni, Kilimani, Michenzani, Gamba, Makunduchi na Bambi (kwa Unguja), pamoja na Chakechake, Mkoani, Kengeja na Wete kisiwani Pemba, kwa kutambua kuwa makaazi bora ni miongoni mwa mahitaji ya msingi katika maisha ya binadamu.
Baadhi ya wafanyakazi wa idara mbalimbali za Mfuko wa ZSSF wakiwa katika hafla ya ufunguzi wa Mradi wa Nyumba za Makaazi za"ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ANGENEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam zilizofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).(IKULU).

Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Kiongozi, Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee (kulia) pamoja na viongozi wengine wakiwa katika hafla ya ufunguzi wa Mradi wa Nyumba za makaazi za"ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ANGENEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam zilizofunguliwa Septemab 21,2020 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.(IKULU).
Pichani ni miongoni mwa nyumba za Mradi wa "ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ANGENEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam zilizofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.(IKULU).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Khamis Mussa Omar alipokuwa akitoa taarifa ya Kitaalam Ujenzi wa Nyumba za Mradi wa "ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ANGENEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam kwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein na wananchi wakati wa hafla ya ufunguzi zilizofunguliwa Septemba 21,2020 Mbweni Magharibi A Unguja. (IKULU)

Waziri wa Fedha na Uchumi, Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein kuzungumza na na wananchi wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Nyumba za Mradi wa "ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ANGENEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam alizozifunguliwa Septemba 21, 2020. (IKULU).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa nyumba za Mradi wa "ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ANGENEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam alizozifunguliwa Septemba 21,2020. Kulia ni Waziri wa Fedha na Uchumi, Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa,Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya ZSSF, Dkt.Suleiman Rashid Mohamed (wa pili kushoto). (IKULU).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein akisoma Jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za ZSSF Mbweni Real Estate, baada ya kuondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi wakati wa hafla ya ufunguzi wa nyumba hizo zilizoko katika eneo la Mbweni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja jijini Zanzibar,kulia kwa Rais ni Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa. (IKULU).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF),Bi.Sabra Issa Machano, wakati akitembelea moja ya nyumba hizo baada ya kuzifungua rasmi Septemba 21,2020 na kushoto kwa Rais ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi. (IKULU).

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar, Khamis Mussa akizungumza na kutoa maelezo ya kitaalam ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za ZSSF Mbweni Real Estate Zanzibar, wakati wa ufunguzi wa nyumba hizo zilizopo katika eneo la Mbweni jijini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi ufungo mmoja wa wanunuzi wa nyumba hizo, Hamid Khamis Othman wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa mradi huo uliofanyika katika viwanja nyumba hizo Mbweni jijini Zanzibar.(IKULU).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi fungo za moja ya nyumba hizo mnunuzi, Talib Mfaume Hassan, wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa nyumba hizo uliofanyika Mbweni jijini Zanzibar.(IKULU).

Ameeleza kuwa, Serikali ya Awamu ya Saba, kama zilivyo awamu zilizotangulia, zimekuwa zikitekeleza juhudi za kuimarisha makaazi ya wananchi, ikiwemo eneo hilo la Mbweni alilosema lina historia kubwa katika nchi.

Alitoa shukurani kwa ZSSF kwa kufanikisha ujenzi huo na kubainisha matumaini yake kuwa hatua ya kuwekeza miradi ya namna hiyo itasukuma mbele maendeleo ya nchi kwa kuinufaisha jamii pamoja na kuleta haiba nzuri ya miji.

“Hongereni ZSSF na uongozi wote wa Wizara Fedha na Mipango, ZSSF inafanya kwa vitendo kuinua mazingira ya wananchi Unguja na Pemba katika Nyanja mbali mbali ikiwemo ya makazi na michezo”, alisema.

Aidha, Dkt. Shein alibainisha kuwa maendeleo ya nchi yoyote ile huonekana kutokana na ujenzi wa majengo na kusema ujenzi wa majengo ya kisasa katika maeneo mbali mbali ya nchi yanatoa taswira ya maendeleo hayo.

Katika hatua nyingine, Dkt. Shein aliitaka ZSSF kuhakikisha kunakuwepo ulinzi katika neo hilo ili kudumisha amani kwa wakaazi wake,na kusema jambo hilo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Vile vile, aliitaka ZSSF kuhamasiha upandaji ya miti ya vivuli katika eneo hilo, kuharakisha ujenzi wa majengo yaliobaki katika mradi huo pamoja na kuvutia wafanyabiashara ili kuanzisha miradi mbali mbali ya utoaji huduma, kama vile kumbi za mikutano na ujenzi wa skuli.

Alitoa shukurani kwa taasisi na watu wote walioshiriki katika utekelezaji wa mradi huo , akiwemo mkandarasi wa mradi ‘Dezo Civil Contactors’.

Mapema, Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa alitoa shukrani kwa Dk. Shein kwa kuitia moyo ZSSF na kufanikisha ujenzi hu na kulifanya eneo hilo kubadilika na kuwa mji mdogo.

Alitoa wito kwa sekta binafsi kuwekeza katika nyanja tofauti za utoaji wa huduma ikiwemo ujenzi wa maduka ili kuwaondolea usumbufu wakaazi wa eneo hilo kufuata huduma hizo masafa ya mbali.

Aidha, aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kusimamaia utekelezaji wa sera ya Taifa katika makaazi, na kubainisha faida mbali mbali zinazotokana na mradi huo ikiwemo za kiuchumi na kijamii.

Nae, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Mipango. Khamis Mussa Omar, alisema mradi wa Nyumba za Makaazi eneo la Mbweni, unaohusisha majengo 15 na vyumba 210, unafanyika kupitia Kampuni ya Kizalendo ya ‘Dezo Civil Contractors’ na pale utakapokamilika utagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 35.

Aliipongeza Serikali kwa kuipatia ZSSF eneo la ziada kwa ajili ya uendelezaji wa miradi yake pamoja na kuupongeza Uongozi uliopita wa taasisi hiyo kwa kuasisi kazi za uwekezaji na uendelezaji wa eneo hilo.Amesema, ujenzi huo utachochea maendeleo na kuimarisha haiba ya nchi.

Katika hafla hiyo ambapo viongozi mbalimbali wa serikali walishiriki, akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein alipata fursa ya kukabidhi funguo na hati za nyumba kwa baadhi ya wamiliki wa nyumba hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news