Wakulima wa parachichi wapewa elimu namna ya kupata matokeo chanya kwa muda mfupi

WAKULIMA wa parachichi katika mji wa Mafinga wilayani Mufindi mkoani Iringa wamepatiwa elimu ya kilimo bora cha zao hilo ambalo hivi sasa lina soko kubwa ndani na nje ya nchi, anaripoti HASSAN NINGA (Diramakini).

Wilson Kashanga akitembelea moja ya shamba la mkulima.

Elimu hiyo imetolewa na Kampuni ya Agrigrow Tanzania Ltd yenye makao makuu yake katika Mji wa Morogoro ambapo wana lengo la kuleta mageuzi makubwa katika kilimo nchini.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara, Wilson Kashanga Mbwambo amasema kuwa, lengo la kuendesha mafunzo hayo ni kuwapatia mbinu za kilimo hicho wakulima ili kuweza kuongeza uzalishaji ambao unakubalika katika soko la Kimataifa.

Hata hivyo, amewataka wakulima hao kuchagua mbegu bora hasa pale wanapotaka kuanzisha vitalu vya miche ya parachichi, kwani hiyo ndiyo hatua muhimu ambayo itamfanya mkulima kupata faida kwa kile anachozalisha.

Wakulima wa parachichi wakiendelea kufuatilia mafunzo ya kilimo cha zao la parachichi kutoka Agrigrow Tanzania.

Katika hatua nyingine ameongeza kuwa, hivi sasa kampuni hiyo itahakikisha wanatoa elimu mara kwa mara sambamba na kuwapatia virutubishi asilia katoka Agrigrow ambavyo vitawaongezea uzalishaji

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Mafinga, Saada Mwaruka amaesema kuwa, katika kuunga mkono uzalishaji wa parachichi hivi sasa wana eneo lenye ukubwa hekari 50 ambazo zitatumika kama shamba darasa kwa wakazi wa mji huo.

Nao baadhi ya wakulima wamesema kuwa, hivi sasa wanakabiliwa na changamoto ya kupata miche bora ya zao hilo ambalo linawangezea kipato kikubwa kutokana na kuwa na soko la uhakika.


Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Agrigrow Tanzania, Wilson Kashanga Mbwambo akizungumza na wakulima wa Parachichi wa Mji wa Mafinga.

Hata hivyo, wameomba elimu hiyo itolewe mara kwa mara pamoja na wataalam kufika katika mashamba ili kuangalia namna wanavyohudumia mashamba yao ya parachichi

Akizungumzia suala la mbegu pamoja na miche bora ya parachichi, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya amesema kuwa, hivi sasa vituo vya utafiti wa kilimo katika mikoa hiyo vimeshaanza kuuza miche ambayo ni bora na yenye kuongeza uzalishaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Mafinga, Saada Mwaruka akizungumza katika mafunzo hayo.

Mafunzo hayo ya kilimo bora cha parachichi yaliyoandaliwa na Kampuni ya Agrigrow Tanzania LTD yenye makao makuu yake katika Mji wa Morogoro yaliweza kuwajengea uwezo wakulima katika kukabiliana na magonjwa na wadudu wasumbufu katika zao hilo pamoja na mbinu za kujikinga nao.

Hata hivyo, wameahidi kuendelea kutoa elimu hiyo kwa wakulima wa mikoa hiyo ya Nyanda za Juu Kusini ili kuweza kuona faida ya kilimo cha parachichi ambacho kitaongeza kipato kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news