WHO:Wagonjwa milioni moja wenye TB, HIV tutawapoteza kutokana na COVID-19

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa, huenda watu milioni moja wenye Virusi vya Ukimwi (HIV) na wanaougua maradhi ya Kifua Kikuu (TB) wakapoteza maisha kutokana na janga la virusi vya Corona (COVID-19) kuwasimamishia matibabu.Hayo yamo katika ripoti ya WHO ambayo ni mpya inayokwenda kwa jina la 'Dunia katika Mparaganyiko' ikiwa ni ripoti ya kila mwaka ya Bodi ya Kutathmini Utayari wa Dunia 2020.

Ripoti hiyo imesema huenda vifo vinavyohusiana na ugonjwa wa Ukimwi zaidi ya 534,000 vikashuhudiwa katika nchi za eneo la chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika ndani ya miezi 12 ijayo.

Ni iwapo walioambukizwa virusi vya HIV wataendelea kukosa matibabu katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa Corona.

Pia ripoti hiyo inakadiria kuwa, vifo 525,000 zaidi vya wagonjwa wa Kifua Kikuu vitasajiliwa mwaka huu 2020, ikilinganishwa na mwaka 2018, kutokana na wagonjwa wa TB kukosa matibabu hali inayochangiwa na COVID-19.

No comments

Powered by Blogger.