Wizara ya Afya:Wazazi chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ni salama, wapeni ridhaa wanafunzi wa kike wapatiwe

Wazazi na walezi hapa nchini wametakiwa kutoa ridhaa kwa wanafunzi wa kike kupata chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi inayotolewa mashuleni.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Ayoub Kibao wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa watoto kupata chanjo

Amesema,changamoto kubwa ipo kwa watoto wa kike ambao wamekuwa wakileta ugumu kwa kukataa kupata chanjo kwa madai kuwa hadi wapate ruhusa ya wazazi au walezi wao.

Amesema,wasichana wengi wapo kwenye hatari kubwa ya kupata saratani ya mlango wa kizazi. 
Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alizindua zoezi la utoaji chanjo,uzinduzi huo ulifanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Sima A na Sima B na kushirikisha watoto wenye umri wa miaka 14 kutoka katika baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari za Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

"Watoa chanjo wanapata wakati mgumu sana wapapofika mashuleni kutoa chanjo, wasichana wengi wanakataa na kusema kwamba hadi wapate ruhusa kutoka kwa wazazi wao,"amesema.

Amesema kuwa, wazazi nao wamekuwa na dhana potofu na hivyo kuwakataza watoto wao kupata chanjo hizo.

Dkt.Ayoub amewahakikishia wanahabari kwamba chanjo hiyo ni salama,hivyo wazazi au walezi wawaruhusu watoto wao kupata chanjo kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huo.

Amesema kuwa, Serikali imejitahidi sana kupeleka chanjo kwa wakati hali iliyosababisha kiwango cha chanjo kuwa juu.

Amesema,Serikali ya Awamu ya Tano kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imenunua magari yenye thamani ya sh.bilioni 700.5 kwa ajili ya kuimarisha huduma za chanjo katika halmashauri 61 hapa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news