Azam FC yaziburuza Simba, Yanga SC Ligi Kuu Bara

Wanalambalamba Azam FC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Mwadui FC mabao 3 kwa surufi usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi wilayani Temeke jijini Dar es Salaam,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kwa sasa inafikisha alama 18 baada ya kucheza mechi sita hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa alama tano mbele ya mabingwa watetezi, Simba na mabingwa wa kihistoria, Yanga ambao hata hivyo wamecheza mechi tano hadi sasa.

Obrey Chirwa aliyefunga mabao mawili 28' na 63' na Prince Dube 61' ndio walioifanya timu hiyo kuendelea kung'ang'ania kileleni kwa alama tano mbele.

No comments

Powered by Blogger.