Benki Kuu ya Tanzania yaonya wanaozusha uongo

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba, huduma za kibenki zinazotolewa na benki na taasisi za fedha nchini zitaendelea kutolewa kama kawaida kwa wateja kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28, 2020, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 15, 2020 na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kwa mujibu wa idara hiyo,Benki Kuu inawataka wananchi kupuuza taarifa potofu zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kwamba kuna maelekezo ya kusitisha huduma hizo muhimu katika kipindi cha uchaguzi.

"Benki Kuu ya Tanzania, kama msimamizi wa benki na taasisi za fedha, haijatoa maelekezo yoyote ya kusitisha huduma za kibenki kwa wateja wa taasisi hizo. Wananchi wataendelea kupata huduma zote za kibenki kama kawaida wakati wote kabla, wakati na hata baada ya uchaguzi.

"Aidha, Benki Kuu inapenda kutoa onyo kwa mtu, watu au kikundi cha watu wenye dhamira ya kupotosha umma na kusababisha taharuki katika jamii kwa kutoa taarifa za uongo. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu, watu au kikundi chochote kitakachobainika kutoa taarifa potofu kwa umma,"imebainisha sehemu ya taarifa ya Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news