Bodi ya Ligi yang'ata mashabiki wa Yanga waliowarushia makonde Wana Simba SC

 

Bodi ya Ligi Tanzania leo Oktoba 2,mwaka huu imeendelea kutekeleza majukumu yake kikamilifu ikiwemo kuchukua hatua kuhusu matukio mbalimbali, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Aidha, wamefanya maamuzi baada ya Kamati ya Kusimamia Ligi Kuu Bara kupitia matukio mbalimbali huku mashabiki wa Yanga SC waliowapiga mashabiki wa Simba SC na kuwachania jezi kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro wakipewa adhabu.

Kwa mujibu wa bodi,adhabu waliopewa ni faini na kufungiwa kutoingia uwanjani kwa muda wa miezi 12  kuanzia sasa.

Post a Comment

0 Comments