Katibu Mkuu wa Chama ACT Wazalendo amshukuru Mungu kwa kuwaepusha na mauti katika ajali

Katibu Mkuu wa Chama ACT Wazalendo,Ado Shaibu amenurika kifo baada ya gari alilokuwa amepanda akiambatana na viongozi wengine jimboni Nanyamba mkoani Mtwara kupata ajali, anaripoti Mwandishi Diramakini (diramakini@gmail.com).

Pichani ni gari ambalo alikuwa amepanda Katibu huyo wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu.

Viongozi hao walikwenda kumnadi Mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Colleta Kadinda. "Wametoka salama kwenye ajali hiyo,"mmoja wa maafisa kutoka ACT Wazalendo amenukuliwa na Mwandishi Diramakini.

Ado Shaibu licha ya kuwa Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo pia ni Mgombea Ubunge Jimbo la Tunduru Kaskazini kupitia tiketi ya chama hicho.

Hata hivyo, Ado Shaibu amesema, anamshukuru Mungu kwa kumnusuru dhidi ya kifo katika ajali hiyo ambayo imetokea leo Oktoba 2, 2020.


Post a Comment

0 Comments